MIILI YA MAREHEMU 13 WA AJALI YA MABASI TABORA YATAMBULIWA


Maiti za watu 13 kati ya 16 waliokufa katika ajali ya mabasi yaliyogongana juzi mkoani Tabora, zimetambuliwa na ndugu zao.
Ajali hiyo ilitokea juzi   saa 8 mchana katika kijiji cha Mlogolo wilaya ya Sikonge baada ya basi ya Am Coach na Sabena kugongana uso kwa uso na kusababisha vifo hivyo na majeruhi 81. 
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora, Suzan Kaganda alitaja waliokufa na maeneo yao ya makazi ni  Patrick Fumbuka , Fred Alex, Emmanuel Senga na Mabaga Benedicto Peter. 
Wengine ni Nicholaus James,  Mkazi wa Geita, Aristideth Shirima dereva wa basi la AM Coach na dereva wa basi la Sabena, James Komba aliyekatika kichwa na kutengana na mwili kwa kukatwa na bati.
Kamanda alitaja wengine ni Jacklini  Lumendika, Nasma Zenda pomoja na mtoto wa kiume.
Alisema katika basi hilo pia kulikuwa na wanafunzi waliokuwa wanakwenda kufanya mtihani katika chuo cha kilimo Tumbi mkoani Tabora wakitoka Mbeya na  Iringa ambao ni Anna Kalimo na Joyce Mgeni.
Kaimu Mganga wa Wilaya ya Sikonge mkoani hapa, John Buswelu alisema  hadi jana, majeruhi 63 waliruhusiwa kutoka katika hospitali ya wilaya hiyo na wengine watatu wanapelekwa Tabora kwa ajili ya matibabu.
Hospitali ya Mkoa Kitete ilipokea wagonjwa wapatao 18 ambao ilionekana hawawezi kutibiwa katika hospitali ya Sikonge.
Akizumzumza na waandishi wa habari jana, Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo ya mkoa wa Tabora,  Deus Kitapondya  alitaja majina ya majeruhi.
Nao ni Meena Shilindye, Silvesta John, Nyorobi Masaga, Salum Hamisi, Athumani Jafari, Samweli Asubisye, Mgeta, Josephat Weya, Paulo Nyanda, Amos Dominick,  Joseph Msumari na Scola Kadati.
Wengine ni Jenifa Sanga,Tora Mbilinyi, Sikujua Saimon na mtoto mwenye umri wa mwaka moja ambaye mzazi wake alifariki. Pia yuko ambaye hawezi kuongea kutokana na ububu.

No comments: