KUPELEKWA NJE KUJIFUNGWA KUTENGENEZA MATANGAZO

Kampuni inayojishughulisha na utengenezaji  wa matangazo ya  Drive Dentsu imepanga kuendeleza wataalamu katika eneo hilo nje ya nchi kuwezesha kupata uzoefu zaidi.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Cheriff Tabet, alisema Tanzania inazo fursa nyingi katika tasnia ya utengenezaji wa matangazo ambapo wataalamu wengi zaidi wanahitajika.
Alisema ili kukidhi soko hilo,  kampuni yake ikiwa ni moja kati ya kampuni kubwa duniani zilizofungua ofisi zake nchini,  ina nia ya kuwekeza zaidi kwa wataalamu hao.
Meneja Mkuu wa Masoko na Maendeleo ya Biashara wa kampuni hiyo, Rami El Khalil, alisema katika kufanikisha malengo yake itatumia zaidi wataalamu wa nchini na nje kuteka soko la matangazo.

No comments: