Kampuni
za simu zimeagizwa kupeleka watumishi wake katika vyuo vya mawasiliano,
kuwezesha utoaji wa huduma bora.
Waziri
wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa alitoa mwito
wakati akifungua mkutano wa 48 wa Taasisi ya Afrika ya Kuendeleza Mawasiliano
(Afralti).
Profesa
Mbarawa alisema teknolojia imekuwa ikibadilika na kukua kwa kasi, hivyo ni
muhimu kwa wadhibiti kuhakikisha wateja wananufaika na teknolojia ya
mawasiliano.
"Kwa
jinsi soko lilivyo kuna umuhimu wa kutoa huduma kwa thamani ya juu, hii
itasaidia sana kuleta maendeleo kwa kasi zaidi kwani bila mawasiliano ni vigumu
maendeleo kuja kwa kasi," alisema Profesa Mbarawa.
Kwa
upande wake, Mwenyekiti wa Afralti, Erwin Mwapasa, alisema taasisi hiyo imekuwa
ikishirikiana na wadau mbalimbali, kuhakikisha teknolojia ya mawasiliano
inatolewa katika kiwango cha juu katika nchi za Afrika.
Alisema
teknolojia ya habari na mawasiliano kwa sasa imekuwa ni muhimu kwa maisha ya
kila siku na imekuwa ikichangia katika maendeleo ya kiuchumi.
No comments:
Post a Comment