KAMPUNI YAMWAGA MSAADA WA SIMU KWA ALBINOJeshi  la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na Kampuni ya Sapna Electronic, imewapatia  simu 20 watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) waishio jijini humo, kwa ajili kuongeza mawasiliano kati yao na jeshi hilo.
Aidha, jeshi hilo limewaasa wenye ulemavu wa ngozi kuwa karibu na jeshi hilo katika kurahisisha mawasiliano kati yao na Wakuu wa Vituo vilivyoko karibu a makazi yao.
Akizungumza juzi, Kamishina wa Polisi Kanda Maalum, Suleiman Kova alisema pamoja na kwamba haijawahi kutokea tukio lolote la ukatili dhidi ya albino, aliwaomba watu hao kuongeza mawasiliano na jeshi hilo.
Aidha alitoa namba zake za simu ambazo ni 0715- 009 983 na 0756 710 197 na kusema kwamba zitumike na maalbino kutoa taarifa za matukio ya uhalifu dhidi yao. Aliongeza kuwa wananchi wote wanaweza kutumia namba hizo kwa ajili ya kutoa taarifa za uhalifu.

No comments: