APANDISHWA KIZIMBANI KWA KUMNAJISI BINTI YAKE WA KUMZAA


Mkazi wa kijiji cha Nyangae, Kata ya Bukumbi wilayani Uyui, Shimba Kajolo ameburuzwa mahakamani akituhumiwa kumnajisi binti yake wa miaka 12.\
Imeelezwa mahakamani kwamba alifanya kitendo hicho kwa kushauriwa na mganga wa kienyeji ili aweze kuondoa mkosi wa kutopata mke. 
Kajolo amefikishwa mbele ya Hakimu Mkazi wa Wilaya ya Tabora, Bahati Chitepo na kusomewa shitaka lake hilo. 
Mbele ya Hakimu Chitepo ilidaiwa na Wakili wa Serikali, Miraji Kajiru kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo Agosti 11, mwaka huu. 
Wakili Kajiru aliiambia mahakama kuwa siku hiyo majira ya usiku Shimba alimnajisi binti yake wa kumzaa (jina linahifadhiwa). 
Mtuhumiwa amekana shitaka hilo na amepelekwa mahabusu baada ya kukosa watu wa kumdhamini hadi Septemba tatu kesi hiyo itakapotajwa.

No comments: