WATU 409 WAKAMATWA KWA UJANGILI SUGU

Watu 409  wanaosadikiwa  kuwa majangili  sugu wamekamatwa wakifanya  ujangili  katika Hifadhi ya Taifa  ya Katavi  wilayani Mlele  mkoa wa Katavi katika kipindi kilichoanzia Juni 2013 hadi Juni mwaka huu.
Katika  kipindi  hicho,  silaha  kadhaa zimekamatwa  ndani ya hifadhi hiyo  ya Taifa  zikiwemo bunduki nzito  aina ya SMG  zipatazo tano,  riffle  G3 zipatazo nane  pamoja na  risasi  zipatazo 357 za SMG.
Silaha nyingine zilizokamatwa katika kipindi  hicho  ni pamoja na bunduki aina ya shotgun zipatazo 21,  bunduki zilizotengenezwa kienyeji “magobori” yapatayo 138.
Mkuu wa Idara  ya Ulinzi  wa Hifadhi ya Taifa ya Katavi, Mhifadhi Davis Mushi wakati akitoa  taarifa  katika kikao cha Kamati ya Ushauri ya Wilaya  ya Mpanda (DDC) iliyoketi mjini hapa.
Alibainisha  kuwa  kuwepo kwa  makazi ya  wakimbizi ya  Katumba wilayani Mlele   na  Mishamo wilayani Mpanda   karibu  na  Hifadhi  ya Taifa ya Katavi  kumesababisha  wakimbizi  wa  makazi  hayo kujihusisha  ujangili  kama  njia  ya kupatia  kipato chao.
Kwa mujibu wa Mushi  uingizaji  kiholela  wa  silaha  mkoani humo  zikipitia mkoa wa jirani wa  Kigoma unafanywa na watu wanaojihusisha  na biashara  haramu  ya meno  ya tembo katika Hifadhi ya Taifa  ya Katavi.
Akifafanua alibainisha kuwa  mtandao  wa watu  kupitia mkoa wa jirani wa Kigoma  na wakibadilishana na  majangili  na meno  ya tembo.

No comments: