Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo ameelezea kufurahishwa na ufaulu mzuri wa wanafunzi wa kidato cha sita katika shule ya Sekondari ya St. Joseph Cathedral inayomilikiwa na kanisa hilo, huku akisikitishwa kuona waliofaulu kwa kiwango cha juu wote ni wavulana.
Kardinali huyo aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam alipotembelewa na wanafunzi walioongoza kitaifa katika masomo ya Sayansi, Sanaa na Biashara wakiongozana na wazazi wao.
Alisema muda wa wazazi kusema mtoto wa kike hana faida sasa umekwisha, watoto wote ni sawa hivyo ni jukumu la kila mzazi kujituma na kuhakikisha mtoto wa kike anapata elimu bora na yenye usawa na mtoto wa kiume.
“Wapo baadhi ya wazazi wanaosema mtoto wa kike hana faida na kazi yake kubwa ni kuolewa na sio kupata elimu wanakosea sana na kuwanyima haki yao ya msingi,” alisema Pengo.
Aliongeza kuwa amefurahi kuona shule yao imefaulisha kwa kiwango cha juu ila angefurahi zaidi kama kungekuwa na msichana aliyeongoza hata mmoja, ila anaamini mwaka ujao ataona wasichana wengi wakiongoza kitaifa.
Pia alisema walifikia uamuzi wa kuwa na shule za makanisa baada ya kuona elimu ya Tanzania imeshuka hivyo waliamua kuungana na makanisa mengine ili watafute njia ya kurudisha elimu iliyoonekana inashuka kwa kasi.
“Tuliamua kila anayeitwa askofu lazima awe na shule angalau moja kuanzia chekechea, sekondari hadi kidato cha sita,” aliongeza Pengo.
Alisema alifurahi baada ya maamuzi hayo walifanikiwa kupata shule za makanisa ambazo zimeonekana kuwa na ufaulu mzuri, na hii ni kutokana na uamuzi walioamua ili kutoa matunda mazuri.
“Kinachotakiwa kwa sasa baada ya ufaulu mzuri ni kulinda ile hadhi na hatutegemei kuona kiwango cha shule kinashuka hata kidogo,” alisema.
Aidha, alisema lengo lao kwa sasa ni kuwa na chuo kikuu na hata ikitokea akafariki, anaamini watakaokuja nyuma wataendeleza mipango ambayo atakuwa ameiacha.
Aliwashukuru wazazi kwa kuweza kuwasaidia watoto hao na kuwajengea nidhamu na ndio maana wapo hapo walipofikia leo, pia aliwapongeza wanafunzi hao na kuwataka kujitahidi zaidi hata waendako ili baadae Taifa lijivunie nao.
Mkuu wa shule hiyo, Sista Theodora Faustine katika maoni yake, alisema amefurahi kuona shule hiyo imetoa wanafunzi waliofaulu kiwango cha juu kitaifa na kuifanya shule hiyo kujivunia.
“Wanafunzi 30 wanakwenda vyuo vikuu, tuna imani tunaweza zaidi tutajitahidi kwa nguvu zetu ili kuendelea kutoa watoto wengi zaidi,” alisema Faustine.
Kwa niaba ya wazazi waliofika katika hafla hiyo, Gwakisa Mwambaja ambaye ni mzazi wa Prince Mwambaja aliyeshika nafasi ya tano kwa wavulana kitaifa katika masomo ya Biashara, alisema wamefurahishwa na elimu bora inayotolewa na St Joseph na kuifanya kuwa juu kitaifa, kitendo ambacho kinawapa furaha kuona watoto wao wanafaulu vizuri.
“Tunalishukuru Kanisa na wewe Kadinali kwa kutupatia shule tuliyoiamini na leo tunafurahia matunda baada ya watoto wetu kufaulu vizuri,” alisema Mwambaja.

No comments:
Post a Comment