Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Dk Binilith Mahenge amekataa kuwapa cheti cha utunzaji wa mazingira kiwanda cha nguo cha Nida kilichopo Tabata katika Manispaa ya Ilala, Dar es Salaam.
Mahenge alisema kampuni hiyo imekosa vigezo wanavyohitaji kwa kuwa maji yake ya viwandani yanatuhumiwa kusababisha kubabuka miguu kwa watoto wanaochezea maji ya mto Msimbazi ambao NIDA wanamwagia maji yao ya kiwandani.
‘’Mlipochunguzwa na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), ilionekana kuwa mmefikia kiwango cha kupata cheti hicho, lakini nimeona kwa macho yangu kuwa mnaidanganya Serikali,’’ alisema Mahenge.
Alisema serikali inahitaji wawekezaji wanaowajali Watanzania na wanaolinda afya zao kwa kutunza mazingira na sio kuwa chanzo cha madhara kwa jamii.
‘’Imenibidi kujiridhisha na hali halisi ya eneo kwani nimeona kuwa hali ya mto imekuwa mbaya kwa kuwa kuna maji machafu yenye rangi tofauti ambayo ni hatari kwa viumbe hai wakati NEMC walinipa taarifa kuwa tayari mmetimiza vigezo,’’ aliongeza.
Kwa mujibu wa Mahenge, kutokana na hali hiyo kiwanda hicho kinapaswa kuadhibiwa kwa kudanganya.
Aidha, alisema kiwanda hicho kina vifaa vya kisasa ila hawataki kuvitumia hadi wasimamiwe na viongozi. Aliwataka kutoa taarifa jinsi gani wataweza kuyabadili maji hayo kwa wakati. Mhandisi Boniventure Baya kutoka Nemc alisema viwanda vyote vinatakiwa kusafisha maji taka wanayozalisha kwa kutumia maabara zilizopo.
Naye Diwani wa Kata ya Kigogo, Richard Chengula alisema wakazi wa eneo lake wanatumia maji hayo kwa ajili ya kumwagilia mboga hivyo maji yanayotoka katika kiwanda hicho yanawaathiri sana. Alisema ni kwa muda mrefu kiwanda hicho kinafungua maji ambayo yana rangi tofauti na kwamba watoto wanaocheza maeneo hayo na wakazi wanaathirika kiafya.

No comments:
Post a Comment