WADAKWA WAKIWA NA HEROIN NA VIFAA VYA KUJIDUNGA

Watu 12 wamekamatwa na dawa za kulevya aina ya heroini yenye uzito wa gramu mbili pamoja na vifaa vya kujidunga wakiwa wamejifungia katika nyumba ya kulala wageni ya Kenios iliyopo maeneo ya Isevya mkoani Hapa.
Watu hao akiwemo mmiliki wa nyumba hiyo ya kulala wageni, walikutwa na vifaa vya kujidungia ambavyo ni sindano na wembe. Watuhumiwa hao ni kutoka maeneo ya Chemchem na Isevya.
Akizungumza na waandishi wa habari  jana Kmanda wa polisi mkoani hapa, Suzan Kaganda alisema kwamba kukamatwa kwa watu hao kumetokana na operesheni zinazoendelea za jeshi hilo la kuwasaka wahalifu katika mkoa wa Tabora.
Tukio hilo lilitokea Julai 23 mwaka huu katika eneo la Isevya baada ya polisi kupewa taarifa na wasamaria wema na ndipo walipofika eneo la tukio.
Kamanda huyo aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Hamisi Athumani (39) , Issa Abdalla (22) Mrisho Shabani (22) wote ni wakazi wa Chemchem. Wengine ni Denis Petro(34), Ramadhani Mbade (40), Haji Abdalla(40) na Devid Malle (43) mmiliki wa gesti hiyo wote ni wakazi wa Isevya .
Wahutumiwa wengine ni Said Kasumari (24) na Shabani Haruna (25) ambao ni wakazi wa mtaa wa Ujiji na Ally Bakari (34), Ramadhani Hamisi na Paschal Robert ni mkazi wa kata ya Ng’ambo.

No comments: