WABUNGE JUMUIYA YA MADOLA WAKUTANA ARUSHA

Mkutano wa  45 wa Umoja wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika (CPA) unatarajia kufanyika kwa wiki moja kuanza leo jijini hapa, huku masuala ya afya ya mama na mtoto, unyanyasaji wa wanawake na ajira kwa vijana vikiwa ni kipaumbele katika mkutano huo.
Hayo yalisemwa jana jijini  hapa na  Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ni Rais wa Umoja wa CPA Kanda ya Afrika, Anne Makinda.
Makinda alisema kutakuwa pia na vikao mbalimbali ukiwemo mkutano mkuu wa mwaka, Kikao cha Kamati ya Utendaji, Mkutano wa Umoja wa Wabunge Wanawake  wa Jumuiya hiyo na makatibu wa wabunge.
Alisema mkutano huo utajadili changamoto mbalimbali  na mafanikio katika utekelezaji wa majukumu yao kitatiba katika kutunga sheria ambapo washiriki zaidi ya 500 kutoka nchi 18 wanatarajia kushiriki mkutano huo.
Alisema moja ya matarajio ya mkutano huo ni kupitisha  mpango mkakati wa CPA Kanda ya Afrika na kuongeza kuwa moja ya vipengele muhimu ni kubariki ujenzi wa jengo la Ofisi ya Kitega Uchumi cha Umoja huo linalotarajia kujengwa eneo la Kigamboni, Dar es Salaam.

No comments: