SILAA ATAKA BUSARA MATUMIZI YA BARABARA DAR

Askari wa Usalama Barabarani wameshauriwa kutumia busara kuwaelewesha madereva wanaoingia katikati ya Jiji la Dar es Salaam kufuatia mabadiliko ya matumizi katika badhi ya mitaa na barabara kuliko kukimbilia kuwatoza faini.
Ushauri huo ulitolewa jana jijini Dar es Salaam na Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa.
Alisema kumekuwa na malalamiko mengi ya watu kusumbuliwa na askari wa Usalama Barabarani kuwatoza faini wakati bado watu hawajaelewa vizuri mfumo unaotumika sasa.
"Nimezungumza na Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani lakini wananchi nao wawe wakali kama hajaona alama amuulize askari, apewe onyo basi sio kila kosa apewe adhabu na isiwe mradi wa watu," alisema.
Aidha alisema ufinyu wa alama za barabarani wanaendelea kukumbushana ziwekwe kuondoa usumbufu huo kwasababu ni kweli alama hizo haziko kila mahali katikati ya Jiji pamoja na mabadiliko yaliyofanyika.

No comments: