AANGUKA GHAFLA NA KUFARIKI DUNIA

Watu wawili wamekufa katika matukio tofauti, akiwemo mkazi wa mtaa wa Tabora na Kariakoo,  Michel Matei , aliyekutwa amekufa baada ya kuanguka ghafla karibu na mlango wa choo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Mary Nzuki alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 4:30 asubuhi, maeneo ya Mtaa wa Tabora kwenye gereji ya Makumba, Wilaya ya Ilala.
Alisema mtu huyo mwenye miaka 65,  alianguka karibu na mlango huo akiwa katika chumba kilichopo kwenye gereji hiyo huku mwili ukiwa hauna majeraha.
Kwa mujibu wa Minangi, mtu huyo alikutwa na cheti cha Hospitali ya  Mnazi Mmoja cha Juni 26 mwaka huu, kilichoonesha vipimo vya mfumo wa damu. Maiti amehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Wakati huohuo, Dereva wa pikipiki Ally Athumani (38) amekufa papo hapo baada ya kugongana na gari la mafuta.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Engelbert Kiondo alisema tukio hilo ni la juzi  saa 11:30 jioni katika barabara ya Kigamboni eneo la Mwembe Mtemvu Wilaya ya Temeke.

No comments: