DALADALA ZA BAISKELI MARUFUKU SHINYANGA

Baraza la Madiwani Manispaa  ya  Shinyanga  limeazimia  kuziondoa  daladala zote za baiskeli  kutokana na  baadhi ya madereva wake  kujihusisha na kufanya vitendo vya kikatili.
Akisoma maazimio ya madiwani hao, Mchumi wa Manispaa hiyo Christopher Nyarubamba alisema madiwani wametaka daladala zote za baiskeli kuondolewa kupelekwa  kando ya mji kwa kusajiliwa na kupewa vitambulisho.
Baadhi ya madiwani akiwemo Diwani Viti Maalumu Shella Mshandete  wameunga mkono azimio hilo na kueleza kuwa  wananchi wa manispaa wanatakiwa kubadilika kama maeneo mengine.
Hata hivyo Diwani mwingine wa Viti Maalumu, Siri Yasin alisema ipo haja ya kutafuta mbadala kwanza wa daladala hizo ili kuondoa dhiki ya usafiri.
Katibu Tawala wa Wilaya, Boniface Chambi  alisema kuwa  daladala za gari zilikuwepo  na uzinduzi ulifanywa na Mkuu wa Mkoa Ally Rufunga  lakini cha kushangaza  watu walikuwa hawazipandi.

No comments: