TRENI YA BARA KUANZA SAFARI ZAKE JUNI 3Treni ya abiria ya Reli ya Kati, inatarajiwa kuanza safari zake Jumanne Juni 3 mwaka huu, baada ya kukamilika kwa ukarabati wa  stesheni za Kilosa mkoani Morogoro na Gulwe mkoani Dodoma.
Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL), umetangaza kuanza kwa usafiri huo jana, baada ya kusitisha usafiri huo tangu Januari 10, 2014.
Mkurugenzi Mtendaji,  Kipallo Kisamfu, katika taarifa yake iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari, aliwataka wananchi wanatumia usafiri huo, wafike katika stesheni zilizo karibu yao tangu jana, kukata tikezi za safari zao.
“Muda wa kuondoka treni kwa siku za Jumanne na Ijumaa kutoka Stesheni ya Dar es Salaam  kwenda Kigoma na Mwanza, utakuwa saa 11 jioni na zile za kutoka Kigoma na Mwanza kuja Dar es Salaam katika siku za Alhamisi na Jumapili, ni saa 11 jioni kutokea Kigoma na saa 12 Magharibi kutokea Mwanza,” alisema.

No comments: