SHINYANGA KUJENGA HOSPITALI YA SHILINGI BILIONI 90Serikali mkoani  Shinyanga  imeanza mikakati ya kujenga hospitali ya rufaa ya mkoa , itakayogharimu jumla ya Sh bilioni  89 .6.
Lengo la ujenzi huo ni kupunguza msongamano    wa wagonjwa katika hospitali na  kuwafanya wananchi  wasisafiri umbali mrefu kutafuta matibabu.
Hospitali hiyo itajengwa katika  eneo lenye hekta 53, sawa na ekari 135 katika kijiji cha Negezi Kata ya Mwawaza.
Eneo hilo ndilo lililopendekezwa tangu awali na kufanyiwa utafiti, ambapo wamiliki wa maeneo haya wamekwishalipwa fidia zilizotengwa za jumla ya Sh milioni 98.
Hayo yalisemwa na Mkuu wa Mkoa wa  Shinyanga,  Ally  Rufunga   mbele ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa.
Alieleza kuwa  fedha hizo ni za mipango ya kuendeleza  majengo na  vitendea kazi. Alisema katika bajeti ya mwaka 2012/13 zilitengwa jumla ya Sh bilioni moja.
Alisema licha ya ujenzi huo kuanza, changamoto  kubwa ni uhaba wa maji. Alisema  Mamlaka ya Maji na Mazingira katika Manispaa ya Shinyanga  (SHUWASA), imeahidi kupeleka maji na kwamba zinahitajika Sh milioni 1.64 kupeleka maji.

No comments: