RAIS KIKWETE ATEUA BOSI MPYA SHIRIKA LA MZINGARais Jakaya Kikwete amemteua Andrew Nyumayo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Mzinga lililopo mkoani Morogoro.
Kwa mujibu wa taarifa ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Job Masima, uteuzi huo umeanza Mei 6, mwaka huu.
Nyumayo amewahi kushika nyadhifa mbalimbali serikalini kabla ya kustaafu, ikiwa ni pamoja na kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.
Sambamba na uteuzi huo wa Mwenyekiti, pia Bodi hiyo itakuwa na wajumbe wafuatao: Luteni Jenerali Samweli Ndomba ambaye ni Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi ambaye katika Bodi hiyo atakuwa Makamu Mwenyekiti, Luteni Jenerali (mstaafu)  Martin Mwakalindile  na  Meja Jenerali Dk Charles Muzanila, ambaye ni  Meneja Mkuu wa Shirika la Mzinga.
Wajumbe wengine ni Meja Jenerali (mstaafu) Said Omar, Meja Jenerali (mstaafu) Festo Ulomi, Kanali Dk Wema Wekwe, John William Nyoka na Adalus Magere.

No comments: