MNYIKA ASAIDIA UJENZI WA ZAHANATI YA MALAMBA MAWILIMbunge wa Ubungo,  John Mnyika ametoa  Sh milioni 10 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa Zahanati ya Malamba Mawili iliyopo Kata ya Msigani katika Manispaa Kinondoni.
Akizungumza na baadhi ya wananchi wa eneo hilo juzi, walioongozwa na Mwenyekiti wao wa Mtaa, Bakari Said (CCM), Mnyika alisema fedha hizo,zinazotolewa kupitia Mfuko wa Mbunge zitaingizwa katika akaunti ya mtaa huokabla ya Juni 30, mwaka huu.
Zahanati hiyo inajengwa kwa ushirikiano wa wananchi wa eneo hilo kwa uchangiaji wa vifaa mbalimbali vya ujenzi, ikiwemo saruji, mabati, nondo, fedha na matofali.
Alisema lengo la fedha hizo ni kuunga mkono nguvu za wananchi wa eneo hiloili kuhakikisha ujenzi huo unakamilika haraka, hivyo kuondoaadha ya wananchi hao kutembea umbali mrefu kwa ajili ya kutafuta matibabu.
Awali, akitoa taarifa fupi kwa Mnyika, Said alisema makadirio yao ujenzi wa zahanati yanaonesha kuwa  Sh milioni 45  zitatumika hadi ujenzi utakapokamilika.
Said alisema hatua ya wananchi wa eneo hilo, kuunganisha nguvu za ujenzi wazahanati hiyo, kumetokana kuchoshwa na adha ya kwenda umbali mrefukutafuta huduma za afya.

No comments: