MKUU WA WILAYA APIGA MARUFUKU STAILI YA "KATA K"

Mkuu wa Wilaya  ya Sumbawanga  mkoani Rukwa, Mathew Sedoyeka  amepiga marufuku   kwa   kijana  yeyote  wa  kiume   mahali popote  wilayani  humo  kuvaa  suruali kwa  staili  ya Kata  K.
Pia  aliwaagiza  viongozi  wa Serikali  za Mitaa , Vijiji , Kata , Tarafa na Wilaya  kushirikiana na Kamati za  Ulinzi  na Usalama  katika maeneo  yao  ya kiutawala  kuwachukulia   hatua kali  vijana wowote  wa kiume watakaobainika  kuvaa  suruali zao kwa  staili  hiyo ya Kata K.
Alitoa  maagizo  hayo  hivi  karibuni  akihutubia  mikutano  mbalimbali  ya hadhara wilayani  humo.
Alisema  tabia  hiyo ya  vijana  wa kiume kuvaa  suruali zao  kinyume cha  utaratibu  haiwezi kuvumilika  kwa kuwa inatukanisha  jamii.
Sedoyeka  alionya  Watanzania  hususani  vijana  kuachana  na tabia  ya kuiga   kila kitu   kutoka  nje ya  nchi   ikiwemo  uvaaji  wa  nguo  zisizo na staha  kwa kuwa  hauendani  kabisa  na mila na desturi  pia maadili  ya Kitanzania.

No comments: