MGOMO WA WAFANYAKAZI TAZARA SASA KIZUNGUMKUTI


Mgomo wa wafanyakazi wa Shirika la Reli la Tanzania na Zambia (Tazara), haujafahamika hatma yake kutokana kikao cha bodi kilichotarajiwa kufanyika juzi au jana kushindikana. 
Mkurugenzi Mkuu wa Tazara,  Ronald Phiri alimwambia mwandishi juzi kuwa kikao hicho cha bodi ya kimeshindikana kufanyika kutokana na baadhi ya wajumbe wa bodi hiyo kushindwa kufika. 
"Kikao hicho kilichotakiwa kufanyika jana au juzi hakitawezekana tena kufanyika, kwa sababu wajumbe kutoka Zambia walisema haingewezekana kupata nafasi ya kuja," alisema Phiri. 
Mgomo wa wafanyakazi wa Tazara ulianza tangu mwanzoni mwa wiki hii wakidai mishahara yao ambayo shirika hilo haijawalipa kwa miezi mitatu. 
Katika mkutano na wafanyakazi Mei 15 mwaka huu, Phiri aliwaomba wafanyakazi kurudi kazini wakati shirika kwa kushirikiana na wabia wa shirika hilo ambao ni Serikali ya Zambia na Tanzania wakishughulikia tatizo hilo. 
Hata hivyo, wafanyakazi walikataa kurudi kazini mpaka pale watakapolipwa mishahara yao.

No comments: