MAGAVANA WA AFRIKA WAKUTANA MJINI KIGALISerikali imesema iko imara katika kuendelea na kusimamia juhudi zinazofanywa na Benki ya Afrika katika kuinua mitaji kupitia mpango wa sita wa kukuza mitaji wa benki hiyo (GCI-VI).
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum alipokuwa akihutubia magavana wa nchi za Afrika katika mkutano wa mwaka wa wadau wa Benki ya Afrika  jijini Kigali, Rwanda.
Alisema  kuwa kupitia mpango wa GCI-VI, Tanzania imekuwa na uwezo wa kulipa hisa zake zipatazo Dola za Marekani 2,683,429.52 katika awamu ya tatu kwa muda uliopangwa.
Alisema kupitia mpango  huo, Tanzania imekuwa mstari wa mbele katika kulipa hisa zake zipatazo Dola za Marekani 2,683,429.52 katika awamu ya tatu kwa muda uliopangwa.
Aidha, Saada alimpongeza Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika,  Dk Donald Kaberuka na uongozi mzima kwa kusimamia na kuongoza kwa umahiri mkubwa majukumu waliyonayo ya kibenki na kuhakikisha inasonga mbele daima na kuifanya kuwa benki bora barani humu.
Rais wa Rwanda, Paul Kagame akifungua mkutano huo, alisema  ili kufikia uchumi wa kati katika Afrika kwa miaka 50  ijayo,  inabidi nguvu kubwa ielekezwe kwenye sekta binafsi ambayo itatengeneza ajira kwa vijana na wanawake. 
Mkutano huo ni wa  siku tano kuanzia 19 hadi 23 Mei mwaka huu. Kabla ya ufunguzi, mkutano huu ulitanguliwa na mikutano mbalimbali ya Magavana ambao ni Mawaziri wa Fedha kutoka nchi mbalimbali barani Afrika, wakifuatana na wajumbe kuwakilisha nchi zao.

No comments: