KITABU CHA "URANI NA MAZINGIRA 2014" CHAZINDULIWA

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora imesema uchimbaji wa madini ya urani bila ya kuwepo sera wala sheria ya kusimamia na kudhibiti shughuli hizo ni jambo la hatari kwa mustakabali wa taifa.
Aidha, imetoa mwito kwa serikali kujipanga vema ili kuweza kuhakikisha makosa ya nyuma hayatojirudia kwani madini hayo ni hatari kuliko madini yotote yaliyowahi kuchimbwa.
Makamu mwenyekiti wa Tume hiyo, Mahfoudha Hamid alisema hayo jana Dar es Salaam wakati akizindua kitabu cha urani na mazingira 2014.
Kitabu hicho kimeandaliwa na Kituo cha sheria na haki za binadamu (LHRC) kwa kushirikiana na taasisi ya Rosa Luxemburg foundation.
Akizungumza, Mahfoudha alisema madini ya urani yana mionzi ambayo isipoangaliwa vyema italeta matatizo katika jamii.
Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa LHRC, Dk Hellen Kijo Bisimba alisema kitabu hicho kitasambazwa nchini kwa lengo la kutoa uelewa kwa wananchi juu ya madini ya urani.

1 comment:

Tajiel Urioh said...

Kweli madhara ni makubwa sana, na jamii itaadhirika kwa kiasi kikubwa, lakini pia najiuliza serikali haioni kuwa mji kama wa dodoma na seleous wakazi wake ni watu muhimu ktk nchi hii?.
Tutandanganywa na wawekezaji tu, mwisho wa siku watatuacha na matatizo.
https://www.facebook.com/thegreenicon