Kampuni
ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL), imepanga kushusha bei ya umeme
kwa Shirika la Umeme (Tanesco), kutoka kati ya senti za kimarekani 26 mpaka 30
kwa uniti moja, mpaka senti sita na nane.
Chanzo
cha habari za uhakika kutoka Wizara ya Nishati na Madini, kilieleza jana kuwa
hatua hiyo, imetishia kupoteza soko kwa kampuni za kigeni zinazozalisha umeme
na kuuza kwa bei ya juu nchini.
Kwa
sasa, kampuni zingine katika soko zinatoza kati ya senti za Kimarekani 38 na 60
kwa kila uniti.
Kampuni
ya PAP iliyonunua IPTL katika taarifa yake kwa vyombo vya habari iliyotolewa
jijini Dar es Salaam jana, imesema Watanzania watafurahia gharama hizo za chini
baada ya utekelezaji wa mkakati wao wa utanuzi na ubadilishaji wa mfumo
wa mitambo yao, ambao utaongeza uwezo wa uzalishaji wa umeme kutoka
megawati 100 za sasa mpaka megawati 500.
Taarifa
fupi iliyotolewa jana na Katibu na Mshauri wa Masuala ya Sheria wa IPTL/PAP,
Joseph Makandege, imesema ikiwa kampuni ya ufuaji umeme, wanaelewa faida za
kiuchumi zitokanazo na umeme wa gharama nafuu kwa mteja mmoja mmoja na kwa
maendeleo ya kiuchumi ya nchi nzima.
No comments:
Post a Comment