HATIMA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA IPO KWA WENYE DHAMANAHatima ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu kwa mujibu wa sheria, iko mikononi mwa waziri mwenye dhamana.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakati akihitimisha michango iliyotolewa na wabunge kabla ya bajeti ya mwaka 2014/15 ya  ofisi yake kupitishwa juzi.
Pinda alisema kwa mujibu wa sheria, umepangwa utaratibu ni wakati gani uchaguzi huo ufanyike kwa kuhesabu miaka mitano tangu uchaguzi uliopita ulipofanyika ambao unaangukia Oktoba mwaka huu. 
“Lakini sheria hiyo hiyo inampa mamlaka waziri mwenye dhamana kuweza kuahirisha hizo tarehe akiona zipo sababu za kuweza kufanya hivyo,” alisema. 
Aliendelea kusema kwamba ikifika wakati ikaonekana iko haja ya kuahirisha tarehe ya uchaguzi huo, watashauriana na Rais na wadau wengine waone namna ya kufanya. 

No comments: