CHADEMA YASAINI MKATABA WA MILIONI 700/- NA DENMARK

Chama cha Demokrasia   na Maendeleo (CHADEMA) kimesaini mkataba wa Sh milioni 700 na Conservative Peoples Party cha  Denmark  ambazo zitasaidia  kuwajengea  uwezo akinamama na vijana katika siasa.
Hayo yalisemwa jana na Katibu Mtendaji katika ofisi ya Katibu Mkuu Victor Kimesera, wakati wa kutia saini mkataba huo Dar es Salaam jana.
“Tunawashukuru sana kwa mchango huu tunaamini utaweza kuwasaidia akinamama wengi na vijana ambao wameonekana kuwa nyuma katika siasa ili na wao wawe na uwezo kisiasa,” alisema Kimesera.

No comments: