BAKITA YABARIKI KWA MUDA NENO UALBINO

Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) limeridhia kutumika kwa muda neno ‘ualbino’ ili kuwatambua watu wenye ulemavu wa ngozi, huku likiendelea kutafiti neno linalofaa kutumika.
Hayo yalisemwa jana na Katibu Mtendaji wa Bakita, Selemani Sewangi baada ya majadiliano yaliyoshirikisha pia maofisa wa Chama cha Watu wenye Ualbino Tanzania (TAS).
“Neno albinism si sahihi kutumika kwa Kiswahili, kwani limetokana na lugha ya Kiingereza, hivyo sio zeruzeru wala wenye ulemavu wa ngozi, ni wenye ualbino, ndivyo tulivyokubaliana kwa sasa,” alisema Sewangi.
Alisema wamekubali kutumia neno ualbino kwa muda, hadi hapo watakapofanya uchunguzi  katika jamii mbalimbali.
Aidha, aliwataka watanzania kutokutazama zaidi tatizo linalowakabili watu hao,  badala yake wawachukulie kuwa ni watu kama walivyo wengine wasio na matatizo ya ngozi.

No comments: