WIZARA YA FEDHA YAIMARISHA MIFUMO YA FEDHA

Wizara ya Fedha  imesema itafanya marekebisho mbalimbali katika bajeti ijayo  ya 2014/2015, ikiwa ni pamoja na kuimarisha mifumo ya fedha.
Pia,  Wizara hiyo imesisitiza matumizi ya mashine za kieletroniki (EfDs).
Hayo yalisemwa jijini Dar es Salaam jana na Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum.
Alisema hayo akati akifungua mkutano wa Baraza la Wafanyakazi ambapo aliwataka kuwa wepesi wa kutoa huduma na kuwa wabunifu, wakifahamu Taifa linategemea wizara hiyo.
Mkutano huo unalenga kupokea taarifa za utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2013/14 na kupokea mapendekezo ya bajeti ya mwaka wa fedha 2014/2015.
Alisema serikali inaangalia bajeti  na Wizara inatakiwa kujitahidi kwa kufanya mambo mara mbili au zaidi,  kutokana na Wizara hiyo kutegemewa zaidi katika kuimarisha uchumi.
wizara hiyo, kutambua  kuwa wanafanya kazi  kwa ajili ya Taifa hivyo waone umuhimu wa kuwa wabunifu, kuwahudumia na kuwasikiliza wananchi wanaofika wizarani wakiwa na mahitaji mbalimbali.
Alisema uchumi wa nchi, unategemea utendaji ulio bora wa wizara hiyo na bajeti ndiyo dira ya kutekeleza majukumu yanayowapasa hivyo wafahamu kuwa wizara ikiyumba nchi nzima itakuwa imeyumba.
Alishauri wafanyakazi kujadili bajeti bila woga kwa kutumia weledi walionao na kutoa ushauri na maoni yatakayosaidia kujenga na kuimarisha wizara katika kutekeleza majukumu iliyojipangia.
Akishukuru, Naibu Katibu Mkuu, Elizabeth Nyambibo alisema wizara itajitahidi kwenda juu ya viwango pamoja na kubadilishana taarifa za kazi ili kuwa wawajibikaji na wawazi.

No comments: