TAESA YASHAURI WANAOTAKA KAZI NJE YA NCHI WAWAFUATE

Wakala wa huduma za Ajira Tanzania (TaESA) umetaka  watu wanaotaka ajira nje ya nchi wapite kwa mawakala hao ili waweze kupata ajira zenye staha.
Hayo yalisemwa jana na msemaji wa wakala Joseph Haule wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Alisema TaESA ni wakala chini ya Wizara ya Ajira na wanahusika na kuunganisha watafuta kazi na waajiri wenye fursa za kazi ndani na nje ya nchi.
Aidha alisema kumekuwa na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi kwamba watu wanaopelekwa nje kufanya kazi wanafanya kazi ambazo zinawadhalilisha na kuwanyima haki zao.
Aliongeza kuwa watu wengi ambao wamekuwa wakipita njia za panya na hivyo matatizo yanapowapata ndio wanalalamikia wakala wakati hawakuhusika katika kuwasafirisha.
Pia alisema mpaka sasa mawakala hao wameshawatafutia kazi watafutakazi 2,614 na wote wapo nje ya nchi na hakuna tatizo lililotokea kwa watu hao mpaka sasa.
Ametoa mwito kwa watafuta kazi wote nchini waweze kujiunga na kupitia mawakala hao ili waweze kutafutiwa ajira zenye staha na ambazo hazitakuwa na matatizo kwao.

No comments: