MWANZA KUZINDUA OPTION B+ APRILI 29

Tume ya Kikristo ya Huduma za Jamii (CSSC) kwa kushirikiana na Ofisi ya Mganga Mkuu mkoa wa Mwanza wanatarajia kuzindua kampeni maalumu ya kutokomeza maambukizi ya virusi vya Ukimwi kutoka kwa mama mjamzito au anayenyonyesha kwenda kwa mtoto (Option B+).
Uzinduzi huo utafanyika Aprili 29, mwaka huu katika viwanja vya hospitali ya rufaa ya mkoa ya Sekou Toure huku Mkuu wa Mkoa wa Mwanza akitarajiwa kuwa Mgeni Rasmi.
Hayo yalielezwa jana na Ofisa Uhusiano wa CSSC, Renatus Sona katika mkutano na waandishi wa habari ambapo alisema kampeni hiyo inatekelezwa kupitia mradi wa ART unaoratibu utokomezaji huo katika mkoa wa Mara, Geita na Mwanza yenyewe.
Alisema CSSC kwa kushirikiana na Wizara ya Afya na inatekeleza mradi huo kwa kutoa huduma za upimaji wa wajawazito, wanaonyonyesha na watoto waliozaliwa na mama anayeishi na virusi vya Ukimwi.
Sona alisema katika kutekeleza Option B+ mkoani Mwanza watoa huduma 557 kutoka vituo vya afya 222 wamepata mafunzo ya kutokomeza maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.

No comments: