MAMBO 10 USIYOYAFAHAMU KUHUSU RAIS ROBERT MUGABE

Robert Mugabe, mwenye miaka 89, bila shaka ni mtu mtata, lakini mengi yanayofahamika ni yale yanayohusiana na maisha yake hadharani. Yote katika maisha yake ya utotoni na ukubwani yameshehenezwa na mishtuko, mengi kati ya hayo yakichagizwa na maamuzi katika awamu zake kadhaa kama Rais wa Zimbabwe. Yafuatayo ni mambo yake 10 ambayo hukuwahi kuyafahamu.
 
1. Wazazi wake wote wawili walikuwa wamejikita mno kwenye dini, na walimlea hivyo kijana wao. Maisha yake yote ya utotoni, alihudhuria shule ya Kijesuti, shukrani kwa  Padri kutoka Ireland ambaye alikuwa mtu aliyemjengea misingi mizuri kabisa katika ujana wake.

2. Mugabe alipoteza kaka zake wakubwa wawili katika umri wa miaka 10. Mmoja alifariki kwa sumum wakati mwingine alifariki muda si mrefu baada ya baba yao kuitelekeza familia hiyo.

3. Wengi wanafahamu kwamba Mugabe kila mara amekuwa mtetezi mkubwa wa elimu. Kiwango cha kujua kusoma na kuandika nchini Zimbabwe kilipanda juu kabisa kuliko nchi yoyote Afrika katika kipindi chake cha urais. Hii ni kwa sehemu kubwa kutokana na ukweli kwamba Mugabe alifanya kazi kama mwalimu wa shule katika kujiandaa na maisha yake ya kisiasa, kwanza akifundisha nchini Ghana (pia alifundisha Zambia) na kisha kurejea Zimbabwe kujiunga na mapinduzi dhidi ya serikali ya weupe ya Rhodesia.

4. Shahada sita za Chuo Kikuu za Mugabe zilipatikana wakati akisoma masomo ya kujiendeleza wakati akiwa gerezani. Yanajumuisha mada zikiwamo elimu, uchumi, utawala, na sheria.
Shahada zinajumuisha Bachelor of Laws and Master’s of Laws kutoka mpango wa elimu ya nje wa Chuo Kikuu cha London, aliyopata wakati akiwa kwenye gereza la Salisbury.

5. Mtoto wa kwanza na wa pekee wa Mugabe aliyezaa na Marehemu Sally Hayfron, Michael Nhamodzenyika, alifariki akiwa na umri wa miaka mitatu kutokana na malaria ya uti wa mgongo mwaka 1966. Mugabe alitaarifiwa kifo hicho akiwa gerezani, na alihuzunishwa mno.

6. Baada ya kuachiwa kwake kutoka gerezani, alitoroka Zimbabwe kwa msaada wa sista wa Kizungu.
Ingawa Warhodesia walimwachia Mugabe kutoka kifungoni, hakutakiwa kuondoka nchini humo. Sista wa Kizungu alimsaidia kuvuka mpana na kwenda Msumbiji, ambako aliweza kujiunga na majeshi ya kimapinduzi.

7. Mwaka 1981, Mugabe alikuwa kwenye orodha ya wanaowania Tuzo ya Amani ya Nobel kutokana na msimamo wake wa kwanza kuhusu maafikiano kufuatia uhuru wa Zimbabwe na kuchaguliwa kwake kuwa Rais wa kwanza wa nchi hiyo. Alisema, "Watu wangu, vijana na wazee, wanaume na wanawake, weusi na weupe, wazima na wafu, mliopo, kwenye tukio hili, muwe pamoja katika muundo mpya wa umoja wa kitaifa ambao unawafanya wote Wazimbabwe."

8. Wakati mkewe wa kwanza akiteseka na maradhi ya saratani, Mugabe akaanzisha mahusiano na katibu muhtasi wake, Grace. Pale ilipobainika kwamba ana ujauzito wa mtoto wake wa kwanza, Mugabe alipuuza maoni ya wengi na kufunga naye ndoa 1996.

9. Umoja wa Nchi za Ulaya ulitoa amri ya kuzuia kusafiri dhidi ya Mugabe ambayo ingemzuia kuingia kwenye nchi yoyote mwanachama wa umoja huo. Hatahivyo, aliweza kukiuka amri hiyo kwa kivuli cha kidini mnamo Machi 2013 ili kuweza kuhudhuria usimikwaji wa Papa Francis nchini Italia.

10. Huku ghasia kadhaa za haki za binadamu zilizosababishwa na Mugabe zikiongezeka, baadhi ya tuzo zake zikabatilishwa. Malkia Elizabeth II alifuta heshima aliyompatia ya kifalme mwaka 2008. Mradi wa kupambana na njaa ukachukua tuzo yake ya Tuzo ya Afrika ya Uongozi kwa ajili ya kukomesha Njaa mwaka 1988. Vyuo vikuu kadhaa vikabatilisha shahada zao za heshima, kikiwamo Chuo Kikuu cha Michigan State, Chuo Kikuu cha Massachusetts, na Chuo Kikuu cha Edinburg.

No comments: