HIZI NDIZO AJALI MBAYA ZAIDI 10 KUWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA

Uchunguzi unaendelea kuisaka ndege ya Malaysian Airlines MH370, ambayo ilipoteza mawasiliano yote na vituo vya kuongozea ndege ikiwa angani kati ya Kuala Lumpur na Vietnam. Siri ya kupotea kwake imeibua hisia nyingi, hasa kufuatia ugunduzi kwamba pasi mbili za kusafiria zilizoibwa zilitumika kupandia kwenye ndege hiyo.Endapo watu wote 239 waliokuwamo ndani wamepotea, itakuwa idadi kubwa kabisa kwa waathirika wa ndege tangu ile ya Septemba 11. Yafuatayo ni maafa mabaya 10 ya ndege katika historia.

1. American Airlines Flight 191

Ajali mbaya kabisa ya ndege katika historia ya Marekani iliyotokea Mei 25, 1979. Ndege iiliyokuwa ikifanya safari zake za kawaida DC-10 ilianguka dakika kadhaa baada ya kuruka kutoka Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa O'Hare mjini Chicago, iliyokuwa ikielekea Los Angeles. Hitilafu za kiufundi zilisababisha injini kwenye bawa la kushoto kujitenga na kuhamia juu ya bawa, kuigeuza ndege hiyo nyuzi 112 na kulazimisha kujibamiza kwenye maegesho ya matrela takribani futi 4,000 kutoka kwenye njia ya kurukia. Abiria wote 271 waliokuwamo ndani na wawili waliokuwa ardhini walikufa. Ndege hiyo DC-10, tayari imejumuishwa kwenye ajali za awali.

2. Ilyushin IL-76

Mnamo Februari 19, 2003, ndege inayomilikiwa na Jeshi la Walinzi wa Wannamapinduzi wa Kiislamu ilianguka kwenye milima karibu na Kerman, Iran, na kuua takribani watu 275 waliokuwamo ndani (baadhi ya ripoti zinasema kulikuwa na majeruhi 2,850). Ndege hiyo ilikuwa imebeba wafuasi wa vikosi maalumu vya Jeshi la Ulinzi la Wanamapinduzi wa Kiislamu. Upepo mkali na ukungu ulidaiwa kusababisha ajali hiyo.

3. Iran Air Flight 655

Ajali nyingine ya kutisha kwa usafiri wa anga nchini Irani, Julai 3, 1988, Iran Air Airbus 300 iliyokuwa ikitokea Tehran kwenda Dubai ikiwa na abiria 290 ilitunguliwa na makombora ya ardhini kutoka kwenye meli ya kivita ya Marekani, U.S.S. Vincennes. Ndege hiyo ilikuwa ikuruka kwenye anga ya Iran wakati huo, na kuzama ndani ya Jangwa la Persian katika eneo la maji la Iran. Marekani ilikiri kufanya makosa na kulipa zaidi ya Dola milioni 61 kama fidia.

4. Saudi Arabian Airlines Flight 163

Wakati moto ambao ulisababisha vifo vya abiria 301 na mfanyakazi ulianzia angani, hii sio ajali ya ndege iliyojumuishwa katika orodha ya zilizosababishwa na matatizo ya kiufundi. Ajali hii ambayo sio ya kuanguka ilitokea Agosti 19, 1980 kwenye Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Riyadh. Moshi uliripotiwa dakika kadhaa baada ya ndege kuwa angani. Rubani alilazimika kutua kwa dharura na ndege ikagusa ardhini. Kwa sababu ambazo hazikufahamika, ndege hiyo iliambaa chini badala ya kuwatoa abiria wake na dakika 23 baadaye, wafanyakazi waliokuwa ardhini wakalizimishwa kufungua milango. Kila mtu aliyekuwamo ndani alifariki kutokana na moshi uliokuwa umetapakaa ndani. Wakati huo, ilikuwa ikichukuliwa kama ajali ya pili ya ndege kwa kuua watu wengi katika historia.

5. Air India Flight 182

Wanaharakati wa Sikh wenye msimamo mkali walishutumiwa kwa mlipuko kwenye ndege ya Air India iliyokuwa safarini kutoka Toronto kwenda Delhi, kupitia mjini London. Ndege hiyo, Boeing 747 ilikuwa imebeba karibu abiria wote raia wa India, ililipuka na kujibamiza kwenye bahari katika anga la Ireland Juni 23, 1985. Kwa zaidi ya miaka 20, mashushushu wa Canada wamekuwa wakitafuta yeyote aliyehusika, huku wakizamisha mamilioni ya dola kwa uchunguzi na majaribio.
Interjit Singh Reyat, raia wa Canada na mfuasi wa wanamgambo wa Sikh Babbar Khalsa, alikiri hatia ya mauaji mwaka 2003 na kuhukumiwa kifungo cha miaka 15 jela kuhusiana na ajali hiyo ya Air India. Pia alidai kuhusika na bomu la pili ambalo lililipuka saa moja baadaye kwenye Uwanja wa ndege wa Narita mjini Tokyo, na kuua watu wawili. Kwenye ndege hiyo, watu 329 walifariki, na kufanya maafa makubwa zaidi katika historia ya Canada.

6. Turkish Airlines Flight 981

Ajali ya anga ya Ermenoville ilipata jina lake kutoka kwenye eneo la tukio ambapo ndege ya McDonnell Douglas aina ya DC-10 ilianguka nje kidogo ya Paris. Bado inachukuliwa kama ajali ya ndege moja iliyoua zaidi ambayo hakuna aliyenusurika katika hitoria. Wengi wa abiria hao 346 walikuwa Waingereza wakiwamo wengi kutoka timu ya vijana ya rugby.
Mnamo Machi 3, 1974, ndege hiyo ilipitia Paris ikitokea Istanbul kuelekea London. Kutokana na migomo, abiria waliokuwa wametelekezwa walizajana kwenye ndege hiyo kupita uwezo wake. Milango ya sehemu ya mizigo kwenye ndege hiyo DC-10 ikabidi ifungwe kwa nje, na wakati ikiwa angani milango hiyo ikafunguka na kuingiza upepo kwa kasi ndani yake kiasi cha kumfanya rubani kushindwa kuimudu.

7. The Charkhi Dadri Midair Collision

Mnamo Novemba 12, 1996 kupita kijiji cha Charkhi Dadri karibu na New Delhi, India, ndege ya Saudi Arabian Airlines aina ya Boeing 747 na Kazakhstan Airlines Ilyushin IL-76 zilibamizana, na kuua watu wote 349 katika ndege zote mbili. Kutofahamu vema lugha ya Kiingereza kwa rubani wa Kazakhstani kulishutumiwa kusababisha kuingia bila ruhusa kwenye anga la ndege la Saudi. Mabadiliko mengi yalifanyika baada ya ajali hiyo, ikiwamo utenganishwaji wa njia za ndege zifanyazo safari za ndani na zile za nje angani.

8. Japan Airlines Flight 123

Idadi kubwa ya vifo kutoka kwenye ajali moja ya ndege ilitokea Agosti 12, 1985, pale ndege ya Japan Airlines aina ya Boeing 747 Flight 123 ilipoanguka kwenye Mlima Takamagahara maili 62 tu kutoka Tokyo - abiria 520 na mfanyakazi waliuawa papo hapo.




9. Tenerife Airport Disaster

Vifo vingi kwenye ajali mbaya zaidi moja ya ndege katika historia ya anga ilitokea kwenye Uwanja wa ndege wa Visiwa vya Tenerife Island Los Rodeos katika Visiwa vya Canary mnamo Machi 27, 1977. Ndege ya Uholanzi ya KLM Flight 485 na Pan Am Flight 1736, zote Boeing 747, zilikuwa zikichangia njia ya kuruka/kutua siku hiyo. Kulikuwa na foleni kubwa iliyotokana na tishio la kuwapo bomu, na ukungu mkubwa uliosababisha kutoonekana vema kwa njia ya kuruka/kutua kati ya rada za ardhini na mnara wa kuongozea ndege. Pale ndege ya KLM ilipojaribu kuruka, ikagongana na ndege ya Pan Am iliyokuwa ikingojea kuruka, papo hapo na kuua watu 248 waliokuwamo ndani ya ndege ya KLM, na 335 waliokuwamo kwenye Pan Am. Kwa bahati, abiria 61, wakiwamo marubani wawili walinusurika ndani ya ndege ya Pan Am.

10. September 11, 2001

Dunia ilishuhudia ndege nne zilizotekwa nyaja zikianguka kwenye maeneo tofauti nchini Marekani, na kusababisha maafa makubwa ya vifo vya abiria 2,907 waliokuwamo kwenye ndege hizo na ardhini. Ndege za United Airlines Flight 175 na American Airlines Flight 11 zilirushwa kuelekea kwenye minara miwili ya World Trade Center, na kuua abiria 140 na watekaji 10. American Airlines Flight ilirushwa kuelekea makao makuu ya jeshi ya Pentagon, na kuua 59 na watekaji watano. United Airlines Flight 93 ilianguka huko Pennsylvania, na kuua abiria 40 na watekaji saba. Osama bin Laden alidai kuhusika na aliuawa nchini Pakistan Mei 2, 2011 na makomandoo wa Marekani.

No comments: