HOFU YA BOMU YAZUSHA KIZAAZAA MKUTANONI ARUSHA

Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema  amelalamikia kitendo cha Polisi Mkoani Arusha, kumzuia kufanya mikutano yake mitatu aliyopanga kuifanya  kwenye  maeneo mbalimbali Jijini hapo, kwa kisingizio cha kuwa hali ya usalama kwa hivi sasa kwa mkoa huo si nzuri.
Lema aliyasema hayo jana Jijini hapa wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari Jijini hapa
Alisema aliomba kibali cha kufanya mikutano na wananchi wa jimbo lake mwezi huu lakini cha ajabu alijibiwa na polisi kuwa hataweza kuruhusiwa kufanya mikutano kutokana na hali za usalama.
Alisema awali alipokea  barua  kutoka polisi ya kuzuiwa kufanya mkutano wake leo ,na kusisitiza kuwa yeye ni mbunge anahaki ya kufanya mikutano na wananchi wake ili kujua kero mbalimbali wanazokutana nazo nay eye kuzishughulikia.
"Wananchi wangu wamevunjiwa nyumba, madiwani wamepigwa na mgambo, mgambo hao hao wanawazuia wananchi wasifanye biashara bado wanakero nyingi sasa naomba kibali polisi wanakataa yani mikutano yangu ndio inasababu za kiusalama lakini kwenye kumbi za starehe na maeneo mbalimbali wanaruhusiwa kufanya mambo yao."
"Polisi nataka wajue ya kuwa mimi ni Mbunge wa kuchaguliwa na wananchi na wananchi wanahitaji kuongea na Mbunge wao halafu wananizuia lakini mimi nasema watake wasitake leo ntafanya mkutano na kama ni kesi wanibambikie maana kama mbunge ninahaki ya kuongea na wananchi wangu ,sasa naomba kibali wanaweka vizuizi hivyo leo nitaongea na wananchi wangu eneo la Kilombero viwanja vya Samunge.
Akizungumzia kuhusu bunge la Katiba ,Lema alisema Bunge hilo badala ya kujadili suala la katiba limekuwa ni bunge la matusi na dhihaka ambalo haliwezi kuendelea kutokana na wajumbe kumshambulia mtu mmoja mmoja badala ya maslahi ya nchi.
Kuhusu kuzuiwa mikutano yake na Jeshi la Polisi alisema aliandika barua kuomba ulinzi Aprili 17 mwaka huu akiomba kufanya mikutano kwenye kata tatu za Manispaa ya Arusha, lakini polisi walimjibu wakisema CCM walishaomba nao Aprili 19 mwaka huu, kufanya mikutano kwenye maeneo hayo aliyoomba yeye kufanya mkutano wake.
"Nashangaa polisi wanazuia mikutano yangu lakini wanaruhusu mikutano ya Injili na starehe katika kumbi mbalimbali, ila mimi kuongea na wananchi wangu wanazui hii haikubaliki na nitafanya," alisema.
Alisema kutokana na kukaa nje ya Jimbo lake kwa muda mrefu na anatarajia kuondoka tena kwa zaidi ya miezi miwili kwa ajili ya bunge la bajeti, alisema ndio sababu kubwa inayomsukuma kuongea na wananchi wake waliokumbw ana mambo mengi ikiwemo bomoabomoa.
Pia sababu nyingine anayotaka kuongea na wananchi wake kutokana na mchakato wa katiba mpya ambao lazima auzunguzie.
Hata hivyo alimpongeza Mkuu wa Mkoa Arusha, Magesa Mulongo kuhutubia wananchi kupitia Redio '5' kuwa hakuna sababu z amsingi za kuzuia mikutano hiyo jambo ambalo alisema ni la kweli.
Naye Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Saba alipoulizwa na waandishi wa habari juu ya kuzuia mkutano wake ,  alisema  wameruhusu baada ya kujiridhisha na hali ya usalama.
"Huko nyuma tulizuia kutokana na hali ya usalama ila sasa tumejiridhisha nimetoka kuongea na OCD kuwa awaruhusu kufanya mkutano na utafanyika leo," alisema Sabas.
Wakati huo huo, Lema alisema bunge la Katiba limekuwa ni bunge la kujadili mtu mmoja mmoja badala ya kujadili suala la katiba na kushangazwa na wabunge baadhi  kuchangia hoja za matusi matusi na dhihaka .

No comments: