BINTI WA MICHAEL JACKSON ABWIA VIDONGE 20 NA KUJIKATA KWA KISU...

Paris Jackson.
Watu wa huduma ya kwanza walikwenda nyumbani kwa Paris Jackson kufuatia ripoti kwamba binti huyo mwenye miaka 15 alimeza vidonge 20 vya dawa ya Motrin na kujikata mwenyewe kwa kutumia kisu cha jikoni, sauti ya simu ya dharura iliyosambazwa juzi inaonesha.

Idara ya zimamoto ya Los Angeles County imetoa sauti ya simu  ikielezea mahitaji ya watu wa huduma ya kwanza kati ya wafanyakazi wake na idara ya uliwali ambao walikuwa wakifuatilia taarifa kutoka nyumbani hapo.
Paris ni binti pekee wa nyota wa muziki wa pop Michael Jackson na alipelekwa hospitali baada ya tukio hilo la Juni 5.
Binti huyo mdogo alielezewa kuwa mwenye fahamu na kupumua wakati simu hiyo ikipigwa, lakini taarifa nyingine kuhusu hali yake au kilichosababisha majeraha hayo zilibaki kwenye simu hiyo, ambayo ilichukua dakika dakika moja.
Perry Sanders Jr., mwanasheria wa bibi yake na mlezi, alisema Paris anaendelea vema na anapatia matibabu muafaka. Hakujibu meseji ya simu ikitaka kujua maoni yake kuhusiana na tukio hilo Jumanne.

No comments: