HATIMAYE BINADAMU MZEE ZAIDI DUNIANI AFARIKI AKIWA NA UMRI WA MIAKA 116...

Jiroemon Kimura (katikati) akiwa na tuzo zake.

Hatimaye binadamu wa mwisho ambaye anaaminika kuwa alizaliwa karne ya 19 amefariki akiwa na umri wa miaka 116.

Jiroemon Kimura, ambaye alizaliwa Aprili 19, 1897, hakuwa tu mtu mzee kabisa duniani bali pia mtu pekee mzee duniani kuendelea kuishi.
Mfanyakazi huyo wa zamani wa posta alifariki katika kitanda chake hospitalini mjini Kyotango, Japan ambako alikuwa akiendelea na matibabu ya nimonia.
Kimura amekuwa akitambuliwa rasmi na Rekodi za Dunia za Guiness kama mtu mzee kabisa duniani aliye hai na mtu mzee kabisa kuwahi kutokea.
Kwa mujibu wa Guiness, Kimura, alikuwa mtu wa kwanza katika historia kuweza kuishi hadi umri wa miaka 116.
Alibahatika kuwa na watoto saba, wajukuu 14, vitukuu 25, na watoto 15 wa vitukuu, vilisema vyombo vya habari vya Japan.
Kwa sasa baada ya kifo cha Kimura, mtu mzee zaidi duniani aliye hai ni Mmarekani James McCoubrey mwenye umri wa miaka 111, ambaye alizaliwa Septemba 13, 1901.
Hatahivyo, babu huyo anayeishi nchini Uingereza anapinga taarifa hizo akidai kwamba ana umri wa miaka 113.
Cheti cha kuzaliwa cha Iran cha Ghahreman Pardis kinasema alikuwa amezaliwa Novemba 2, 1903, na kumfanya kuwa na miaka 109 lakini familia yake inasema nyaraka zake zilirekebishwa mara mbili hivyo kumwezesha kupata huduma za bure.
Wanasema kwa hakika alizaliwa mwaka 1899, ambayo inamfanya kuwa na umri wa miaka 113 na siku 69.

No comments: