SIR ALEX FERGUSON ABWAGA MANYANGA MANCHESTER UNITED...

Muda mfupi uliopita, Meneja wa Manchester United Sir Alex Ferguson ametangaza rasmi kwamba atastaafu klabuni hapo mwishoni mwa msimu huu baada ya kuiongoza klabu hiyo kwa miaka 27.

Meneja huyo mwenye miaka 71 amebeba ubingwa wa 13 wa Ligi Kuu akiwa na klabu hiyo mwezi uliopita, lakini hiyo itakuwa chereko yake ya mwisho kama meneja wa klabu hiyo ya Old Trafford.
Tetesi zilmekuwa zikizagaa kwamba Mskochi huyo angehitimisha majukumu yake ya muda mrefu klabuni hapo, lakini mabosi wa Manchester United wamekataa kuzungumzia suala hilo.
Sir Alex alisema katika taarifa yake kwamba ilikuwa muhimu kwake kuiacha klabu hiyo 'ikiwa imara iwezekanavyo.'
Alisema: "Uamuzi huo wa kustaafu ni pekee niliofikiria kushughulikia na pekee ambao sikuuchukulia kiwepesi. Ni wakati muafaka.
"Ilikuwa muhimu kwangu kuondoka hapa ikiwa imara kabisa na naamini nimefanya hivyo.
"Ubora wa kikosi hiki cha ushindi wa ligi, na uwiano wa umri ndai yake, unahakikisha muendelezo wa mafanikio katika kiwango cha juu sambamba na muundo wa maandalizi ya vijana yatahakikisha kwamba hatima ya muda mrefu ya baadaye ya klabu inabaki na nuru."
Sir Alex atabaki kuwa sehemu ya uandaaji katika Old Trafford licha ya kubwaga manyanga katika mambo ya ndani ya uwanja.
Atachukua majukumu kama Mkurugenzi na Balozi wa klabu hiyo wakati atakapostaafu baada ya mechi ya Machester United dhidi ya West Brom itakayochezwa Mei 18 - ikiwa ni mechi yake ya 1,500 kuiongoza klabu hiyo.
Ferguson ameshatwaa mataji 49 katika kipindi chake chenye mafanikio kama meneja nchini Uingereza.
Mataji hayo ni ST MIRREN: (Daraja la Kwanza Scotland: 1976-77), ABERDEEN: (Ligi Kuu ya Scotland: 1979-80, 1983-84, 1984-85), Kombe la Scotland (1981-82, 1982-83, 1983-84, 1985-86), Kombe la Ligi Scotland (1985-86), Kombe la Washindi Ulaya (1982-83), Super Cup ya Ulaya (1983), MANCHESTER UNITED: (Ligi Kuu England: 1992-93, 1993-94, 1995-96, 1996-97, 1998-99, 1999-2000, 2000-01, 2002-03, 2006-07, 2007-08, 2008-09, 2010-11, 2012-13), Kombe la FA: (1989-90, 1993-94, 1995-96, 1998-99, 2003-04), Kombe la Ligi: (1991-92, 2005-06, 2008-09, 2009-10), Ngao ya Jamii: (1990, 1993, 1994, 1996, 1997, 2003, 2007, 2008, 2010, 2011), Ligi ya Mabingwa: (1998-99, 2007-08), Kombe la Washindi Ulaya (1990-91), Super Cup Ulaya (1991), Kombe la Mabara (1999), Kombe la Dunia la FIFA kwa Vilabu (1999).

No comments: