NDEGE YENYE ABIRIA 297 YASINDIKIZWA NA NDEGE ZA KIVITA BAADA YA TISHIO LA UGAIDI...

Ndege hiyo ya Shirika la Pakistan International Airlines baada ya kutua salama.
Ndege za kivita za RAF zilipigania na kuingilia ndege iliyokuwa ikiwasili kutoka Pakistan juzi huku kukiwa na hofu za uwezekano wa kutekwa ndege hiyo.

Ndege hizo mbili za Typhoon zilichanja mbuga angani kuikabili ndege hiyo ya Shirika la Pakistan International Airlines kufuatia ripoti kuwa wanaume wawili 'walijaribu kuingia katika chumba cha marubani'.
Baada ya rubani kubonyeza kitufe cha dharura, waliisindikiza ndege hiyo huku ikiwa imebadilishwa uelekeo kutoka Manchester, ambako ilikuwa imebakiza dakika kumi tu itue, na kuelekezwa uwanja wa Stansted ulioko mjini Essex.
Tukio hilo halikufikiriwa kuwa linahusiana na ugaidi, lakini hali ya hewa wiki hii imechafuka kufuatia mauaji ya mwanajeshi huko Woolwich hivyo kuzifanya mamlaka husika kutoacha mwanya wowote.
Maofisa wa polisi wenye silaha kutoka polisi wa Essex waliingia kwenye ndege hiyo aina ya Boeing 777 na kuwakamatwa wanaume wawili raia wa Uingereza, wenye umri wa miaka 30 na 41, kwa tuhuma za 'kuhatarisha usalama wa ndege hiyo'.
Ndege hiyo ya PIA yenye namba PK709 ilikuwa imebeba abiria 297 na wafanyakazi 11 katika safari hiyo ya masaa 13 kutoka mjini Lahore, Pakistan kwenda Manchester.
Abiria mmoja, Umari Nauman alisema: "Wafanyakazi wa kwenye ndege hiyo walituarifu kwamba kwa kifupi walitaka kuingia chumba cha marubani muda mchache na sababu walishakataliwa kufanya hivyo wakaanzisha majibizano na wafanyakazi hao na kutoa vitisho kiasi.'
Rubani Nadeem Sufi aliripoti kwa wakubwa zake makao makuu ya PIA nchini Pakistan kwamba, dakika 30 kabla ya kutua, wafanyakazi wa kwenye ndege hiyo walimweleza kwamba abiria wawili waliwatishia 'kulipua ndege hiyo baada ya mabishano makali'.
Rubani huyo aliripotiwa kusema: "Mara baada ya kunieleza, nikabonyeza king'ora kwa chumba cha usalama wa anga." Alituma kile kinachofahamika kama 'squawk 7700' - namba za dharura zinazotumwa na alama za radio kuashiria ndege iko katika hatari.
Ndege hizo haraka zikaruka kutoka RAF Coningsby mjini Lincolnshire, kama tahadhari.
Abiria mwingine, Noman Rivzi alisema baadaye: "Hatukugundua chochote kisicho cha kawaida hadi tulipoona ndege ya kivita nje kwenye dirisha.
"Rubani huyo alitutangazia kwamba tumebadili uelekeo kwenda London kufuatia hali mbaya ya hewa. Pale ndege hiyo ilipotua, rubani akatueleza tulikuwa kwenye tishio na kwamba ndio sababu tukasindikizwa na  ndege za kijeshi."
Kwa zaidi ya miaka 30, Stansted umekuwa uwanja wa ndege maarufu kwa utekaji na matukio makubwa ya usalama, ukiwa na eneo lililojitenga likifahamika kama Compass Base pembezoni mbali kutoka uwanja huo mkubwa.
Mapema baada ya kutua, askari wenye silaha walivamia ndege hiyo na kuwakamata wanaume hao wawili. Walitambuliwa na maofisa wa PIA kama Umera Ashraf na Mohammad Shafqat, raia wa Uingereza wenye asili ya Pakistan ambao walikuwa  kwenye daraja la kawaida katika viti namba 81J na 61H.
Abiria waliobakia waliambiwa waache mizigo yao na walisindikizwa kutoka kwenye ndege hiyo. Walipelekwa katika eneo maalumu wakati polisi na wataalamu wa milipuko wakiikagua ndege hiyo.

No comments: