HILI NDILO BAO LA ARJEN ROBBEN LILILOIPA BAYERN MUNICH UBINGWA WA ULAYA 2013...
Mabingwa wa soka nchini Ujerumani, Bayern Munich usiku wa kuamkia leo imetawazwa kuwa mabingwa wapya wa Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kuwachapa Borussia Dortmund mabao 2-1 katika mechi ya fainali iliyowakutanisha miamba hao wawili wa Ujerumani kwenye Uwanja wa Wembley, nchini Uingereza. Hiyo ilikuwa fainali ya pili kwa Bayern Munich katika kipindi cha miaka mitatu, ambapo ilishuhudia mchezaji mwenye kasi ya ajabu Arjen Robben akiwapa raha mashabiki wake hao kwa kufunga bao la ushindi dakika ya 90 ya mchezo, baada ya kuwasononesha katika fainali zilizopita dhidi ya Chelsea. Katika fainali zilizopita, Robben alikosa penalti ambayo ilikuja kuigharibu timu hiyo kwa kukosa ubingwa.
Comments