CHEKA TARATIBU...

Ili kumdhibiti mkewe, jamaa mmoja akabuni mtindo ambao aliamini kwamba ni dawa tosha. Kila siku anapokuwa kazini mida ya mchana lazima apige simu, na mambo yakawa hivi.
Mume: "Uko wapi?" Mke: "Nipo nyumbani baby!" Mume: "Kama kweli, hebu washa blenda!" Mke akiwasha tu basi jamaa roho kwatu akiamini kweli yuko nyumbani. Siku moja jamaa akashitukiza kurudi nyumbani na kumkuta msichana wa kazi peke yake. Jamaa akauliza: "Mke wangu yko wapi?" Msichana akajibu: "Katoka tangu asubuhi akiwa kabeba blenda!" Kasheshe...

No comments: