Hatimaye mgogoro wa uongozi katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Kaskazini Kati Arusha, umeanza kupata muafaka, baada ya Halmashauri Kuu ya Dayosisi kutengua amri ya kumfukuza kazi Mchungaji Philemoni Mollel wa Usharika wa Ngateu na kumrudisha kazini bila masharti yoyote.
Jana katika Usharika wa Ngateu Mtaa wa Kiranyi, Mchungaji Mollel alitambulishwa rasmi katika ibada ya misa ya pili, iliyoanza saa 4.35 asubuhi, iliyokuwa ikiongozwa na Msaidizi wa Askofu mstaafu wa Dayosisi ya Kaskazini Kati Arusha, Mchungaji Gabriel Kimirei.
Mchungaji Mollel alifukuzwa kazi katika Kanisa hilo kuanzia Desemba 24, kwa kile kilichoelezwa kuwa ni makosa yasiyovumilika ndani ya kanisa.
Kabla ya kufukuzwa kazi Mchungaji huyo, kuliibuka mgogoro katika kanisa hilo baada ya moja ya benki za biashara (jina tunalo), kuipa Dayosisi hiyo muda hadi Desemba 31 mwaka jana, iwe imelipa deni la Sh bilioni 11, vinginevyo mali zake zingepigwa mnada.
Kutokana na taarifa hiyo ya benki, kanisa lilitoa waraka wa Askofu ambapo waumini zaidi ya 600,000, walitakiwa kila mmoja achangie Sh 20,000, ili kunusuru mali za kanisa zilizokuwa hatarini kufilisiwa baada ya hoteli ya Corridor Springs, mali ya kanisa hilo, kudaiwa fedha hizo.
Baada ya waraka huo, baadhi ya waumini akiwamo Mchungaji Mollel, walitaka waliohusika na uzembe uliosababisha deni hilo, wawajibike kabla ya waumini kutoa mchango huo.
Kutokana na msimamo huo, Mchungaji Mollel alitakiwa kuomba radhi na alipokataa, alisimamishwa kazi na kuvuliwa madaraka ya kuhudumia Usharika wa Ngateu aliokuwa akihudumia.
Kabla ya kuanza ibada, wachungaji na wazee wa kanisa kutoka katika sharika zaidi ya 10 za Dayosisi hiyo, na wageni wa ndani na nje ya nchi, waliandamana kumwingiza kanisani Mchungaji Mollel, kwa nyimbo za dini zenye kutaka amani ndani ya kanisa.
Mara baada ya kufika ndani ya kanisa, madhabahuni, Mchungaji Kimirei alifanya mambo mawili, kwanza alizindua madhabahu na mimbari kwa kuweka wakfu, na pili alimtambulisha na kumrudisha rasmi katika Usharika wa Ngateu, Mchungaji Mollel.
Akihubiri mbele ya mamia ya waumini wa kanisa hilo, kutoka katika mitaa mitano ya usharika huo, Mchungaji Kimirei aliwataka waumini wa kanisa hilo, wainjilisti na wachungaji, kutomchukia mtu kwa yote kutokana na yaliyotokea.
Mchungaji Kimirei alisema miongoni waliokuwepo kanisani hapo, sio wote wanaopenda Mchungaji Mollel kurudishwa kazini, lakini ni wachache, na aliwataka waumini hao kubadilika na kujiunga upande ulioshinda.
‘’Hapa kanisani kuna zaidi ya asilimia 99.9 ya waumini waliofurahia na kufarijika na ujio wa Mchungaji Mollel kwa mara nyingine, na asilimia 0.1 ndio haifurahii, lakini ukiona umeshindwa katika vita, jiunge na upande wa ushindi,’’ alisema Msaidizi wa Askofu mstaafu na kupigiwa makofi.
Mchungaji Kimerei alisema kuwa Mchungaji Mollel alirudishwa kazini kuanzia Mei 2 mwaka huu, kwa barua rasmi kutoka kwa Kaimu Mkuu wa Dayosisi ya Kaskazini Kati Arusha, Mchungaji Solomoni Masangwa.
Kurudishwa kazini kwa Mchungaji Mollel, kunatokana na uamuzi wa kikao cha Halmashauri Kuu ya Dayosisi ya Kaskazini Kati Arusha, kilichoketi Mei Mosi mwaka huu.
Akisalimia kanisani hapo, Mchungaji Mollel aliwataka waumini kutulia na kuwasamehe wale wote waliokuwa mstari wa mbele kusaliti kanisa na kuleta mgogoro usio kuwa na tija kwa kanisa.
Mchungaji Mollel ambaye alisitishwa mara kwa mara kuzungumza na waumini waliokuwa wakipiga vigelegele, shangwe na vifijo, alisema mara zote haki ya mtu haidhulumiwi wala haiyumbishwi na mtu, bali hucheleweshwa.
‘’Sasa naomba wote kwa pamoja tuache yote yaliyopita, tushirikiane kwa nguvu zote kulijenga Kanisa hili bila ya kuyumbishwa kwa kasi ile ile,‘’ alisema.
Mmoja wa waumini wa kanisa hilo, Emmanuel Mbise, alisema siku zote uongo hujitenga na ukweli, na mwisho wa uongo ni aibu.
Mbise alisema baadhi ya viongozi wa juu wa Dayosisi, walikuwa wakimpotosha Askofu Thomas Laizer (sasa marehemu), kwa kuficha maovu yao, lakini sasa Mungu ameona na ametenda mema kwa Mchungaji Mollel kurudishwa kazini.
Mbali ya hilo, kikao hicho kikubwa katika Dayosisi kilimuachisha kazi Katibu Mkuu wa Dayosisi hiyo, Israel ole Karyongi, na kumwagiza kukabidhi ofisi hiyo mwishoni mwa mwezi huu, kwa Katibu mpya aliyeteuliwa kukaimu nafasi hiyo, Mchungaji Gideon Kivuyo, ambaye ataanza kazi rasmi Juni mosi mwaka huu.
Kivuyo ni Mwenyekiti wa Misioni na Uinjilisti wa Dayosisi ya Kaskazini Kati Arusha.
Uamuzi mwingine uliotolewa na Halmashauri Kuu hiyo ni kuvunja Bodi ya Wakurugenzi ya Hoteli ya Corridor Spring, iliyokuwa ikiongozwa na Katibu Mkuu Karyongi, na kumteua Onesmo Metili kuwa Mwenyekiti mpya wa bodi hiyo mara moja, ambaye pia alikuwepo katika misa ya kumrudisha Mchungaji Mollel.
Halmashauri hiyo pia imemuondoa Katibu wa Kamati ya Mchakato wa Kumpata Katibu mpya wa Dayosisi hiyo, Godwin Lekashu kwa madai ya kukosa sifa na kumteua Mchungaji Profesa Joseph Parsalawe, ambaye ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Makumira, kushika nafasi hiyo.
Pia, kikao hicho kilitengua amri ya Karyongi ya kufunga akaunti ya Usharika wa Ngateu katika Benki ya NBC, na kuamuru ifunguliwe mara moja.

No comments:
Post a Comment