JAJI ASHITAKIWA KWA KUIBA VIDHIBITI VYA DAWA ZA KULEVYA...

Paul Pozonsky.
Jaji mmoja ameshitakiwa kwa kuiba dawa za kulevya aina ya cocaine za ushahidi katika kesi alizoziendesha nchini Marekani.

Paul Pozonsky, mwenye miaka 57, alidaiwa kuficha dawa hizo baada ya kuwataka polisi kuzileta katika chumba cha mahakama kutumika kama vidhibiti.
Mei mwaka 2012, wapelelezi wa polisi walipekua ndani ya bahasha zenye vidhibiti na kugundua cocaine imehamishwa au kuibwa.
Baadhi ya pakiti zilikuwa zimejazwa hamira na zilikuwa na alama za vipimo vya DNA za jaji huyo wa Mahakama ya Washington.
Pozonsky - ambaye alianzisha mahakama ya tiba ya dawa za kulevya iliyobuniwa kusaidia watu kuepuka jela kwa makosa ya dawa za kulevya - alijiuzulu mwaka jana.
Anakabiliwa na orodha ndefu ya mashikata ikiwamo wizi, kumiliki na kuvunja uaminifu kwa mali aliyokabidhiwa na alishitakiwa juzi.
Mwanasheria wake Bob Del Greco alisema: "Hii inaleta matatizo. Hii inaumiza kama unavyoweza kutarajia. Na ni jambo zito na analichukulia kama hivyo."
Katika moja ya matukio Pozonsky anadaiwa kumwita ofisa wa polisi aliyekuwa akishughulikia kesi moja na kumtaka alete mzigo wenye jumla ya zaidi ya gramu 200 za cocaine kwenye mahakama yake.
Wakati fulani, alitaka apelekewe vidhibiti vyote kwa ajili ya kesi moja lakini baadaye akarejesha vitu ambavyo havikuwa dawa za kulevya - ikiwamo fedha taslimu na kitara.
Habari hiyo imevuta hisia na maoni lukuki katika mtandao wa Facebook, ukiwamo mmoja kutoka kwa Michele Pozonsky ambao ulisema: "Nimeolewa katika familia ya Pozonsky miaka 18 iliyopita, wazazi wa Paul ni watu wakarimu katika dunia hii na alikulia katika familia nzuri ya Kikristo.
"Simwombei msamaha, kama alifanya hicho wanachosema, basi natumaini alifanya wakati huo. Lakini msituhukumu wengine tuliobaki kwa sababu yake, kila familia ina mmoja wetu aliyeko katika jicho la jamii."

No comments: