Evarist Mangala. |
Mtuhumiwa
sugu wa matukio ya unajisi na vitendo vya kikatili dhidi ya watoto,
anashikiliwa Polisi mkoani Shinyanga, baada ya kukurupushwa katika jaribio la
kutaka kumnajisi na kumtoboa macho mwanafunzi mwenye umri wa miaka minane.
Kamanda
wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga, Evarist Mangala alisema ofisini kwake jana,
kuwa mtuhumiwa huyo, Jacob Mayani (28), ameshanajisi watoto wanne wa umri wa
kati ya miaka minane hadi 10 na kuwatoboa macho.
"Mayani
anatuhumiwa kunajisi na kuwafanyia ukatili wa kutoboa macho watoto wanne wenye
umri wa kati ya miaka nane hadi 10, kwa lengo la kutaka kuvuruga ushahidi ili
wasimtambue,’’ alidai Kamanda Mangala.
Kwa
mujibu wa madai ya Kamanda Mangala, mtuhumiwa alikamatwa mwishoni mwa wiki
kwenye shamba la mahindi katika mtaa wa Mwasele Manispaa ya Shinyanga, baada ya
jaribio lake la kutaka kumnajisi mtoto mmoja kushindwa.
Inadaiwa
jaribio hilo lilishindwa baada ya mtoto aliyekusudiwa kunajisiwa, kufanikiwa
kuponyoka mikononi mwa mtuhumiwa na kutimua mbio huku akipiga kelele za kuomba
msaada.
Kutokana
na kelele hizo, Kamanda Mangala alisema
wasamaria wema walijitokeza wakamkamata mtuhumiwa na kumfikisha kituo
cha Polisi.
Kamanda
Mangala alisema mtuhumiwa alifanya unyama huo
katika muda usiozidi mwezi mmoja katika matukio na maeneo tofauti ya
Kitangili, Ndembezi na Ndala.
Alisema
watoto wawili kati yao, walilazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando na mmoja
hospitali ya Mkoa wa Shinyanga.
Kwa
mujibu wa madai hayo, madaktari walitoa taarifa Polisi kwamba jicho la mmoja wa
watoto hao limeharibika baada ya kutobolewa.
Kamanda
Mangala alisema baada ya kumkamata mtuhumiwa huyo jana, watoto wawili waliopata kufanyiwa unyama huo,
walifika kwenye kituo cha Polisi mjini hapa na kumtambua mtuhumiwa kwenye
gwaride la utambulisho.
Alisema
mtuhumiwa ni mkazi wa mshikamano katika
manispaa
ya Shinyanga na hujishughulisha na kazi ya kutoa huduma ya usafiri wa baiskeli,
maarufu kwa jina la bodaboda na uuzaji wa urembo.
Inadaiwa
mtuhumiwa alikuwa akirubuni watoto hao
kwa
kuwapa mahindi mabichi ya kuchoma na mavazi ya kubana au vipodozi vya urembo.
Kamanda
wa Polisi alisema kutokana na tabia na
mwenendo
wa mtuhumiwa, inahofiwa kuna watoto wengi waliofanyiwa vitendo hivyo, lakini
kwa sababu moja au nyingine wazazi au watoto hawajaripoti matukio hayo.
Kamanda
huyo alitoa mwito kwa wazazi na walezi, kutoa taarifa kama watoto wao
walinajisiwa na mtuhumiwa.
Mtuhumiwa anashikiliwa na Polisi na baada ya uchunguzi
kukamilika, atafikishwa mahakamani kujibu mashitaka yanayomkabili.
No comments:
Post a Comment