Rais Jakaya Kikwete ameelezea kushtushwa na taarifa za kifo cha aliyekuwa Mwekahazina wa Taifa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Alfred Tandau.
Mzee Tandau, ambaye ni kiongozi wa miaka mingi wa wafanyakazi na Waziri wa muda mrefu wa Serikali, aliaga dunia juzi jioni katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) mjini Dar es Salaam, ambako alikuwa amelazwa kwa matibabu ya saratani ya tumbo.
Katika salamu zake kwa Katibu Mkuu CCM, Abdulrahman Kinana, Rais Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM, alisema amepokea kwa mshituko na masikitiko taarifa za kifo cha Mzee Tandau.
“Nakutumia wewe Katibu Mkuu wa CCM, Mheshimiwa Kinana salamu zangu za dhati za rambirambi kuomboleza msiba huu. Aidha, kupitia kwako nawatumia rambirambi viongozi na wanachama wote wa CCM kwa kumpoteza kiongozi na mwanachama mwenzetu.
“Aidha, kupitia kwako, naomba ufikishe salamu nyingi za pole kwa familia kwa kuondokewa na kiongozi na mhimili wa familia. Wajulishe kuwa niko nao katika kuomboleza kifo cha kaka yetu na kiongozi mwenzetu na naelewa machungu yao katika kipindi hiki. Napenda wajue kuwa naungana nao kumwomba Mwenyezi Mungu aiweke peponi roho ya marehemu. Amina,” alisema Rais Kikwete.
Alisema alimfahamu Alfred Tandau kwa miaka mingi. Alikuwa kiongozi hodari na mwaminifu ambaye katika nafasi zote alizozishikilia katika utumishi wake wa umma, alithibitisha uadilifu na uzalendo wa kiwango cha juu.
“Katika uongozi wa Chama cha Wafanyakazi (NUTA) na baadaye Juwata, Mzee Tandau alijipambanua kuwa mtetezi halisi na mkweli wa maslahi ya wafanyakazi. Katika Serikali ambako alitumika miaka mingi kama Waziri, alikuwa mwaminifu na mtii kwa Serikali yake, kwa viongozi wake na kwa wananchi aliowatumikia,” alisema Rais Kikwete.
Alisema katika nafasi yake ya Mwekahazina wa CCM, aliendeleza sifa hizo hizo alizokuwa nazo tangu awali. “Tutakosa sana busara na ushauri wake.”

No comments:
Post a Comment