WAFANYABIASHARA WAVAMIA STENDI KUU YA DALADALA UBUNGO...

Ni kweli kwamba kila mmoja hutafuta riziki yake kwa namna yake, lakini unapokosekana utaratibu mzuri hali hii hugeuka kero kama walivyonaswa abiria hawa ambao walikuwa wakihaha kutafuta sehemu salama ya kusubiria mabasi ndani ya stendi hiyo jana jioni. (Picha zote na ziro99blog).
Abiria huyu akilazimika kupita sehemu ambayo hupita mabasi jana jioni kutokana na wafanyabiashara kuhodhi njia nzima ya abiria na waenda kwa miguu ndani ya stendi hiyo.
Imekuwa shida hata kupata sehemu ya kusimama kwa usalama kutokana na ongezeko kubwa la wafanyabiashara ambao hufanyia shughuli zao sehemu wanazopaswa kusimama abiria na hivyo kusababisha msongamano usio wa lazima.

No comments: