KIJANA WA KIZUNGU ALIYEWEKWA UTUMWANI NA FAMILIA YA WEUSI AKUTWA AMEKUFA...

KUSHOTO: Happy Sindane wakati alipokuwa na miaka 16. KULIA: Sindane akiwa kazini kuhudumia mifugo.
Mtu mmoja ambaye aliwahi kudaiwa kuwa mtoto wa kizungu anayetumikishwa na familia ya watu weusi amekutwa ameuawa, dhahiri ikiwa kwa kupigwa mawe hadi kufa.

Happy Sindane alikutwa amekufa juzi katika kijiji cha Tweefontein, akiwa 'ameshambuliwa vibaya', polisi walisema.
Hakuna yeyeote aliyekamatwa na inasemekana haijafahamika lengo la mauaji hayo.
Msemaji wa polisi Leonard Hlathi alisema: "Watu ambao walikuwa wakipita waliuona mwili huo uliokuwa umelala kwenye mitaa huko Tweefontein.
"Kulikuwa na mawe yaliyokutwa eneo la tukio. Inaonesha kama alikuwa amepigwa mawe hadi kufa."
Mwaka 2003, Sindane alikwenda kituo cha polisi karibu na Pretoria na kudai alikuwa ametekwa kutoka familia ya watu weupe miaka 12 kabla na amekuwa akiishi kwenye mji wa watu weusi.
Sindane, wakati huo akiwa na miaka 16, alisema alikuwa akidhalilishwa na kulazimishwa kuishi nje akichunga mifugo.
Amefungua madai kimataifa kutafuta wazazi wake halisi lakini shauri hilo la miezi minne mwaka huo lilitaja kwamba jina la kuzaliwa la Sindane lilikuwa Abbey Mziyaye na kwamba alikuwa mtoto wa kiume wa mfanyakazi wa ndani mweusi, Rina Mzayaye.
Mahakama hiyo iligundua baba yake anawezekana kuwa mtu mweupe, Henry Nick, ambaye alimuajiri Mzayaye mwaka 1983, mwaka ambao alizaliwa kijana wao huyo.
Familia yake ya watu weusi ilisema walimchukua mtoto huyo aliyekuwa hahitajiki, aliyetelekezwa na mama yake, na kumchukulia kama mmoja wao.
Sindane alikuwa amegongwa na basi dogo na gari baada ya kulala barabarani mwaka 2004, iliripotiwa. Haikuweza kufahamika kwanini alikuwa barabarani hapo.
Mwaka huohuo, alifikishwa mbele ya hakimu mjini Pretoria baada ya kudaiwa kurusha mawe na kuvunja kioo cha taksi lakini baadaye alifutiwa mashitaka hayo.
Kwa mujibu wa taarifa, binamu wa Sindane, Thomas Kabini, ambaye alikuwa akiishi naye katika kijiji cha Tweefontein, alisema alikuwa 'mwenye kujituma na mcheshi' mara ya mwisho alipoongea naye Alhamisi.
Alisema: "Nilikwenda kutambua mwili wake. Kichwa chake kilikuwa kimejeruhiwa vibaya. Sehemu iliyobaki ya mwili wake ilionekana kutodhurika."
Alisema hakuna maandalizi yoyote ya mazishi yaliyokwishafanyika.
Jacqui Mofokeng, mmoja wa wadhamini wa Mfuko wa Happy Sindane, ambao umeanzishwa kwa fedha kutoka Dulux baada ya kutumia picha yake bila ruhusa, alisema Sindane alikuwa 'mvulana wa majanga'.
Alisema mara ya mwisho aliongea naye miaka miwili iliyopita.
Alisema: "Wakati huo alikuwa akifanya kazi ya udalali wa magari mjini Benoni. Nilimtaka anieleze kwa undani kuhusu udalali huo na mmiliki huyo alinihakikishia atamtunza Happy."
Mofokeng alisema sehemu kubwa ya familia ya Sindane walishakufa na alikuwa akiishi na jamaa za mama yake mlezi wa zamani Betty Sindane.
Alisema: "Bila kujua wewe nani na wapi unapoweza kukaa katika jamii si kazi rahisi kwa kila mmoja".

No comments: