CAF YAIPA TAIFA STARS POINTI 3 DHIDI YA IVORY COAST, SASA YAONGOZA KUNDI...

Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars'.
Ndoto za Tanzania kushiriki fainali za Kombe la Dunia nchini Brazil sasa zimekaribia kabisa kutimia baada ya Shirikisho la Soka la Afrika (CAF) kuinyang'anya timu ya Ivory Coast ushindi ilioupata dhidi ya Taifa Stars katika mchezo wa kwanza uliochezwa mjini Abidjan, nchini Ivory Coast.
Kwa mujibu wa taarifa zilizowekwa kwenye mtandao wa Shirikisho hilo jana, Ivory Coast imepokwa ushindi huo baada ya CAF kujiridhisha kwamba Taifa Stars ilitendewa vitendo visivyo vya kiungwana wakati walipokuwa nchini humo.
Ikifafanua suala hilo, CAF kupitia mtandao huo imeeleza kwamba Taifa Stars ilifikia hata kunyimwa chakula hotelini, kufungiwa huduma ya maji na kuzimiwa umeme nyakati za usiku.
Kama haitoshi, taarifa hiyo ya CAF ilisema kwamba Taifa Stars ilipewa uwanja mdogo wa kufanyia mazoezi ambao una ukubwa wa kutosha magari madogo mawili tu.
Kwa uamuzi huo, Ivory Coast imenyang'anywa pointi zake tatu na mabao mawili ilizopata katika mechi hiyo iliyochezwa mapema mwaka jana, na kupewa Taifa Stars.
Hivyo sasa Taifa Stars inaongoza kundi hilo kwa kuwa na pointi 9 ikifuatiwa na Ivory Coast yenye pointi 4, Morocco pointi 2 na Gambia inayoshika mkia kwa kutokuwa na pointi yoyote.

Leo ni Aprili Mosi - Siku ya Wajinga Duniani!

No comments: