BINTI WA KAHABA ASHINDA FIDIA SHILINGI MILIONI 52 KWA MATESO YA UTOTONI...

KUSHOTO: Collette alivyo sasa. KULIA: Akiwa amebebwa na mama yake wakati akiwa na umri wa miaka mitatu.
Binti wa kahaba ameshinda fidia ya malipo ya Pauni za Uingereza 20,000 baada ya kushitaki ustawi wa jamii kwa kushindwa kumpeleka kwenye matunzo ya kudumu wakati alipokuwa mdogo ili kumnusuru kutoka kwa mama yake mwenye maneno makali.

Collette Elliott, mwenye miaka 35, alifungua mashitaka dhidi ya ustawi wa jamii mjini Birmingham mwaka jana, katika kile kinachodhaniwa kuwa kesi ya kwanza ya aina yake nchini Uingereza.
Collette, kutoka Erdington, Birmingham, alimudu kuweka kumbukumbu zake za ustawi wa jamii ambazo zilionesha maofisa kwamba walikuwa wakifahamu fika kuhusu tabia ya mama yake, Maureen Batchelor.
Maureen, ambaye alifariki kutokana na uvimbe kwenye ubongo Agosti, mwaka jana, alionywa kwa kumtongoza, uharibifu wa kihalifu na kwa kushindwa kumlisha binti yake ipasavyo.
Ustawi wa jamii walimtaarifiwa kwanza kuhusu tabia ya mama yake pale Collette alipokuwa na umri wa miezi miwili tu, na walishiriki kikamilifu kumweka katika uangalizi mara mbili kabla ya kufikisha miaka minne.
Pia walifahamu kuhusu wapenzi wahalifu wa Maureen, misuguano yake na sheria na tabia yake ya kutokuwa na makazi maalumu mara kwa mara.
Collette, ambaye sasa mwenye furaha akiwa ameolewa, alieleza: "Nilikuwa mtoto aliye kwenye hatari na waliniacha kwenye uangalizi wa wazazi wasiostahili na wasiotunza.
"Naamini habari yangu itasaidia watu wengine walioathiriwa na mfumo kujitokeza na kupata haki yao. Nilisalimika mateso yangu, lakini baadhi ya watoto hawana bahati."
Mwaka 1977, mgeni mmoja wa afya aliripoti Maureen alikuwa akimlisha binti yake mlo wa maziwa ya mgando, viazi na mchuzi, na kwamba mtoto huyo mara kwa mara alifikishwa hospitali kutokana na maambukizi.
Alipotimiza miaka 14, Collette alieleza Ustawi wa Jamii Birmingham mama yake alikuwa akimng'ata na kumpiga na hivyo kuaomba kurejeshwa kwenye sehemu za kulelea watoto lakini hakuna hatua zozote zilizochukuliwa.
Wakati fulani wafanyakazi wa ustawi ambao waliwapata wazazi kwa ajili ya kumuasili na walipendekeza kwamba asirejeshwe kwa mama yake ilitenguliwa.
Collette aliweweseshwa na utoto wake kwamba kwa umri wa miaka 18 alijaribu kujiua mwenyewe. Alifanya majaribio 12 kwa zaidi ya kipindi cha miaka 10 iliyofuata huku akipambana na shikinikizo la kisaikolojia.
Akizungumza mwaka jana alisema: "Ilikuwa mwaka jana, baada ya kuonana na daktari wa saikolojia, ndipo nilipoamua kutafuta nini hasa kilichonitokea kwa kusoma makabrasha ya Ustawi wa Jamii yanayohusiana na maisha yangu ya utotoni.
"Nilihisi kuumwa wakati nakiyasoma. Kwa bahati kila kitu kikakaa mahali pake, na kujihisi nilisalitiwa. Nilimchukia mama yangu."
Ustawi wa Jamii Birmingham umeshindwa kukiri makosa yoyote. Msemaji mmoja alieleza: "Maamuzi ya kazi za jamii huwa magumu pale unapokuwa unakabiliana na hukumu inayohusisha kuwaondoa watoto kutoka kwa wazazi wao.
"Katika kesi hii halmashauri haikukubali kwamba maamuzi yake hayakuwa sahihi. Hatahivyo, kesi hiyo imemalizwa kwa misingi ya ushauri wa kisheria."
Collette kwa sasa anashughulikia matakwa yake ya kuombwa radhi.

No comments: