UMOJA WA ULAYA KUCHUNGUZA KUFUNGIWA GAZETI LA MWANAHALISI...

Nchi  za Umoja wa Ulaya kwa kushirikiana na Ujerumani wanafanya uchunguzi wa kufungiwa kwa magazeti nchini ili kuweza kupata uhakika na kushauri serikali pale panapofaa.
Hatua hiyo inafanywa ili kujenga uhusiano na jamii kuhusu utata uliopo wa kuona baadhi ya magazeti kufungiwa, likiwamo gazeti la kila wiki la MwanaHALISI.
Balozi huyo aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Maadhimisho ya miaka 50 ya Idhaa ya Kiswahili  ya Radio Deutsche Welle (DW) yatakayofanyika kesho jijini Dar es Salaam.
Alisema  uhuru kwa vyombo vya habari katika nchi unasaidia katika maendeleo ya nchi na jamii husika huku ikikuza demokrasia na waandishi wa habari wakifuata misingi ya taaluma yao.
Akizungumzia maadhimisho hayo, Mkuu wa Idhaa ya DW, Andrea Schmidt alisema wameamua maadhimisho hayo kufanyika nchini kutokana na kuwa na wasikilizaji wengi wanaowapa mrejesho kwa kutuma ujumbe au kupiga simu baada ya vipindi katika watu milioni 86 wanaopokea habari toka idhaa hiyo kila wiki.
“Kesho mchana tutafanya maadhimisho haya ya uandishi wa habari uliotukuka kwa lugha ya Kiswahili  katika Jengo la Makumbusho ya Taifa kwa kuwaunganisha wachambuzi wanaoheshimika katika mjadala wenye maudhui  ya  ‘Maarifa na Mwamko kupitia vyombo vya Habari,” alisema.
Alisema jopo la majadiliano  hayo lililotayarishwa kwa msaada wa Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) utaongozwa kwa Kiswahili na Mohammed Khelef wa idhaa hiyo na kuwashirikishwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari, Maelezo, Assah Mwambene na Mwandishi wa Habari, Jenerali Ulimwengu.
Wengine ni Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa Habari wanawake (TAMWA), Valerie Msoka na Mtaalamu wa Mitandao ya kijamii, Maggid Mjengwa huku kukiwa na waandishi wa Idhaa hiyo kutoka Rwanda, Burundi, Uganda, Kenya, Kongo na Tanzania.

No comments: