JINSI BABA MTAKATIFU MPYA ANAVYOPATIKANA...

St. Peter's Basilica.
Makardinali wa Kanisa Katoliki wanaotafuta mrithi wa Papa Benedict XVI watafanya mkutano wa faragha kuchagua Baba Mtakatifu mpya siku chache zijazo.
Ni makardinali pekee ndio wanaruhusiwa kwenye mkutano huo wa faragha, ambao utaendelea hadi mrithi atakapochaguliwa.
Makardinali hao watakutana ndani ya kanisa dogo la Vatican na kufanya awamu mbili za upigaji kura kwa siku hadi watapomchagua Papa mpya ikiwa ni theluthi mbili ya wote.
Kwa utamaduni wao walikuwa wakifungiwa kwenye kanisa dogo, maarufu zaidi kwa dari lililochorwa sanamu na ukuta wa madhabahu uliochorwa na Michelangelo, na hawaruhusiwi kutoka nje hadi wamemchagua Baba Mtakatifu mpya.
Walilazimika kulala kwa zamu kwenye vizimba na kuchangia vifaa vichache vya usafi
Lakini taratibu mpya zilizoanzishwa na Papa Yohanne Paul II mwaka 1996 ziliwaruhusu kuishi katika hoteli mpya iliyojengwa kwenye viwanja vya Vatican nyuma ya St. Peter's Basilica na hata kutembea kwenye bustani tulivu za ikulu kati ya awamu za upigaji huo wa kura.
Mabadiliko mengine yamewapa nafasi makardinali kuamua kwa kura ya jumla endapo hawakufanikiwa kumchagua papa baada ya takribani wiki mbili za upigaji kura.
Mikutano ya faragha ya sasa yamedumu kwa siku chache tu. Wakati makardinali wakiwa kwenye makubalino, mmoja aliyechaguliwa atasema 'Accepto,' moshi mweupe, utachomoza kutoka kwenye chemli, kengele zitalia na kardinali atatokeza kwenye dirisha la katikati la St. Peter's Basilica kutamka 'Habemus papam' - "Tunaye Papa".

No comments: