Baadhi ya wakazi wa Dar es Salaam wakishuhudia magari yaliyoangukiwa na ukuta huo jana. |
Watu wanne wamejeruhiwa na magari 24 yaliyokuwa yameegeshwa katika maegesho ya Stendi Kuu ya Mabasi yaendayo Mkoani Ubungo (UBT) yameharibiwa baada ya kuangukiwa na ukuta.
Ajali hiyo ilitokea jana Saa 11: 40 alfajiri, baada ya ukuta uliokuwa unabomolewa kuangukia magari yaliyokuwa yameegeshwa katika eneo hilo.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela aliyekuwepo katika eneo la tukio alisema chanzo cha ajali hiyo ni ukuta ambao ulianza kubomolewa na kwamba majeruhi wamepelekwa katika Hospitali ya Palestina iliyopo eneo la Sinza, Kinondoni kwa ajili ya kupatiwa matibabu.
Akizungumza na mwandishi, mmiliki wa pick-up yenye namba za usajili T 293 AWP, Masauni Mtandika ambaye mwanaye alijeruhiwa, alisema alifika eneo hilo Saa 11 alfajiri kwa ajili ya kumsindikiza mke wake na mtoto wake waliokuwa wanakwenda mkoani Tanga kwenye msiba.
Alisema walipofika hapo mtoto wake alisema anataka kwenda kujisaidia lakini kabla hajafungua mlango alisikia kelele baada ya mwanaye kufunikwa na kifusi ambapo alimuokoa na kwa sasa yupo hospitali.
“Inasikitisha sana kwani inasemekana tangu juzi walikuwa wanabomoa maegesho haya, lakini cha ajabu wakati tunafika hapa wafanyakazi hawakutuelekeza badala yake kibao na mshale vilikuwa vinaonesha kuwa tunatakiwa kuegesha hapa,” alisema Mtandika.
Kwa upande wake, Nelson Wichungura alisema haamini kilichotokea kwa kuwa wakati anafika alikuwa ameegesha sehemu nyingine lakini wafanyakazi wa pale walimwambia akapaki pale na cha kushangaza juzi walikuwa wanabomoa lakini hakuna alama iliyokuwa ikionesha eneo hili ni hatari.
Kwa upande wake Meneja wa kituo hicho, Juma Iddi alisema wakandarasi walimwambia eneo hilo ni salama na hivyo hawezi kutoa taarifa kwa sasa mpaka apate ripoti kutoka kwao.
Mbunge wa Jimbo la Ubungo, John Mnyika (Chadema), aliwataka wananchi kuwa wavumilivu na kuwapa ushirikiano ili kuondoa magari hayo na kuongeza kuwa ajali hiyo imesababaishwa na uzembe na amewasiliana na meneja ambaye ameomba aondoe magari kwanza ndipo wazungumze.
Wananchi walioshuhudia tukio hilo walisema wakandarasi hao wanafanyakazi bila kujali maisha ya watu, wanachojali ni fedha tu.
“Watu hawa waliopaki sio kama hawana akili bali waliambiwa na wafanyakazi wa manispaa waegeshe hapa na mtu akiegesha tofauti gari lake linafugwa kwa minyororo mpaka alipe faini Shilingi 80,000 na pesa hizo anachukua yeye,” alisema Juma Abdalah.
Magari yaliyoangukiwa ni yenye namba T 310 CCU aina ya Toyota Noah; Toyota Rav4 T 423; Suzuki T 932 CAQ; Toyota Noah T 591 BTN; Hyundai T 126 BJM; Toyota Salon T 529 ABS; Pick-Up T 293 AWP; Land Rover T 403 AHT; Bajaji T 724 CAG; Toyota Cresta T 547 CAY; Toyota Corolla T 362 AEW; Nissan March T 304 CAH; Toyota Noah T 625 BQC; Pick-Up T 408 CES; Toyota Vitz T 803 BKX; Toyota Starlet T 170 APE; na Toyota Ceres T 804 AGC.

No comments:
Post a Comment