Msanii Elizabeth Michael 'Lulu'. |
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imepanga Ijumaa Januari 25 mwaka huu, kusikiliza maombi ya dhamana ya msanii wa filamu, Elizabeth Michael ‘Lulu’ anayekabiliwa na mashitaka ya kumuua Steven Kanumba bila kukusudia.
Lulu ambaye bado yupo rumande aliwasilisha maombi ya dhamana kupitia kwa jopo la mawakili wake, Kennedy Fungamtama, Peter Kibatala na Fulgence Masawe, kwa kuwa shitaka lake linadhaminika.
Mawakili hao waliwasilisha maombi hayo chini ya hati ya dharura wakitaka maombi hayo kusikilizwa na kuamriwa mapema kwa madai kuwa mshitakiwa amekaa rumande kwa muda mrefu.
Awali kesi hiyo ilifunguliwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu katika hatua za awali huku Lulu akikabiliwa na mashitaka ya kumuua msanii mwenzake Kanumba kwa kukusudia.
Hata hivyo baada ya upelelezi kukamilika, Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) alibadilisha mashitaka dhidi yake na kuwa ya kuua bila kukusudia, ambapo Desemba 21 mwaka jana, alisomewa maelezo ya kesi na ushahidi utakaotumika.
Kesi hiyo ilihamishiwa Mahakama Kuu na kusajiliwa kama shauri la kuua bila kukusudia, lenye namba ya usajili 125 ya mwaka jana na kupangiwa kusikilizwa mbele ya Jaji Zainab Mruke.
Kwa mujibu wa hati ya maombi iliyoambatanishwa na hati ya kiapo cha wakili Kibatala, wanaiomba Mahakama iamuru mshitakiwa apewe dhamana, akiwa au bila kuwa na wadhamini, au kutoa masharti ambayo Mahakama itaona yanafaa.
Katika hati hiyo Wakili Kibatala anadai mshitakiwa anaweza kutimiza masharti ya dhamana yatakayotolewa na Mahakama na pia anawadhamini wa kuaminika ambao wapo tayari kufika mahakamani kwa niaba yake.
Wakili Kibatala anadai kwa muda ambao ameiendesha kesi hiyo amemfahamu vyema Lulu pamoja na familia yake na anajua kuwa muombaji huyo ana tabia nzuri na ni wa kuaminika.
Aliongeza kuwa Lulu bado yuko chini ya uangalizi wa wazazi wake ambao wako tayari kuhakikisha anatimiza masharti na anafika mahakamani atakapohitajika. Pia ni mtu maarufu hivyo ni rahisi kufuatilia dhamana yake.
Lulu anadaiwa kuwa Aprili 7 mwaka jana katika eneo la Sinza Vatican alimuua Kanumba bila kukusudia.
Upande wa mashitaka unatarajia kupeleka mashahidi tisa pamoja na vielelezo ikiwemo ramani ya eneo la tukio kwenye chumba alichofia Kanumba, na ripoti ya uchunguzi wa kifo pamoja na maelezo ya onyo ya Lulu.

No comments:
Post a Comment