ALIYEMVUA HIJABU MWANAMKE AHUKUMIWA KIFUNGO JELA...

Kijana mmoja jambazi amehukumiwa kifungo jela kwa kushikiri kwake katika shambulio la kibaguzi ambalo mwanamke  kutoka Sudan alivuliwa hijab lake alilojifunga kichwani.
Paige Bain mwenye miaka 16, pia alimpiga ngumi mara kadhaa mwanamke mwenye ujauzito wa miezi mitano wakati wa shambulio hilo, ambalo alilifanya akishirikiana na shangazi yake, Eileen Kennedy mwenye miaka 28.
Umaimi Musa kutoka Darfur, nchini Sudan na rafiki yake kutoka Congo, Mary Marandran walikuwa wameketi kwenye bustani ya michezo mjini Royston, Glasgow, Septemba mwaka jana pale waliposikia mdomo mchafu wa mbaguzi huyo ukiporomosha matusi dhidi yao.
Tukio hilo lilinaswa na kamera za CCTV na muongozaji kamera huyo alitoa taarifa kwa polisi huku tukio hilo likitendeka.
Juzi, Liwali Kenneth Mitchell alimhukumu Bain kifungo cha miaka miwili na miezi minane jela kwa shambulio hilo.
Hapo kabla Kennedy alishahukumiwa kifungo cha miaka miwili na miezi sita kwa kuwa sehemu ya shambulio hilo. Shangazi huyo ambaye wakati huo alikuwa na miaka 15 na Kennedy, walipatikana na hatia wakati wa usikilizwaji wa shauri hilo mapema katika Mahakama ya Uliwali ya Glasgow kwa  kumshambulia Umaimi mwenye miaka 41 na kumsababishia majeraha.
Kennedy pia alikiri kukataa kukamatwa na kudai alikuwa ameathirika kabla ya kumfokea ofisa wa polisi.
Bain alikiri kuongezea kipigo hicho cha ubaguzi kwa Mary, mwenye miaka 40.
Mwendesha mashitaka msaidizi Mark Allan, akisoma mashitaka alisema: "Bain, alimtandika ngumi kwa kurudia-rudia kichwani Mary ambaye wakati huo alikuwa mjamzito na kumsukuma."
Aliieleza mahakama kwamba wote walidaiwa kuitaka simu ya mkononi ya Umaimi na kujaribu kuinyakua kutoka kwake baada ya  kuwaambia kwamba anawapigia simu polisi.
Allan alisema Umaimi alipigwa ngumi kichwani na kuanguka chini.
Aliongeza: "Akiwa kalala chini, alipigwa mara kadhaa ngumi za kichwani na kwenye mwili wake.
"Hijab lake au kilemba - kama kilivyoonekana akiwa amejifunga wakati wa shambulio hilo - kilivutwa kutoka kichwani mwake, na aliporwa simu yake ya mkononi.
"Maofisa wa polisi walielekezwa eneo la tukio na wote waliokuwa wakiongoza kamera hizo za CCTV."
Wote Mary na Umaimi walipelekwa kwenye zahanati ya Royal iliyoko mjini Glasgow kwa matibabu.

No comments: